NA HADIJA OMARY
Idadi ya watalii kutoka mataifa mbalimbali wanaofika katika Hifadhi ya Urithi wa Utamaduni wa Dunia wa Magofu ya kale Kilwa Kisiwani na Songo Mnara imeongezeka imeonekana kuongezeka mara tatu zaidi kutoka wageni 300 mwaka 2023 hadi kufika zaidi ya 900 mwaka 2024
Akizungumza wakati wa mapokezi ya meli ya nane ya kitalii iliyo na jumla ya wageni 125 msimamizi wa utalii kanda ya kusini mashariki chini ya Mamlaka ya usimamizi wa wa wanyamapori Tanzania TAWA huko wilayani kilwa Kamishina msaidizi wa uhifadhi Saidi Mshana
Amesema mafanikio hayo yametokana na jitihada zinazofanywa na serikali kupitia mamlaka hiyo kwa kuhakikisha inaimarisha miundombinu ya barabara kutoka kivutio kimoja na kingine pamoja na sehemu za mapumziko zinakuwepo
"Lakini pia gati kuhakikisha mali zile zikifika boti zile zikifika zinashusha wageni kwa usalama zaidi na kuweza kuingika katika kivutio hiki ambacho ni kikubwa katika uridhi wa Dunia "
"Kipekee nimshukuru sana Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa ajili ya maboresho haya ambapo kwa kiasi kikubwa yamewezesha mafanikia haya ya ujio wa watalii wengi kutoka mataifa mbalimbali "
Mkuu wa hifadhi hiyo ya Urithi wa Utamaduni wa Dunia wa Magofu ya kale Kilwa Kisiwani na Songo Mnara Mercy Mbogelah amesema toka mamlaka ya wanyama poli Tanzania Tawa kuanza kufanya maboresho na kuvutia wageni wengi kufika katika vivutio hivyo vya kihistoria wenyeji waishio katika mji huo wa kitalii wameanza kunufaika katika shughuli mbalimbali
Amesema wenyeji na wajasiliamali wamekuwa wakijipatia kipato kutokana na shughuli mbalimbali kama vile biashara za vitu pamoja na fursa za kuwatembeza watalii hao.
0 Comments