Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Askofu wa kanisa Katholiki Jimbo la Njombe Eusebio Kyando amewataka wakatholiki waliojaaliwa kufunga katika kipindi cha Kwaresma na kisha kufungua wakati wa Pasaka kuendelea kuyatenda mema badala ya kujiingiza kwenye matukio ya kihalifu,Ulevi wa kupindukia na uovu mwingine.
Askofu Kyando ametoa kauli hiyo mara baada ya misa ya Siku kuu ya Pasaka katika Kigango cha Nazareth Mjini Njombe ambapo anasema Watanzania wengi wamekuwa na mazoea ya kudhani baada ya mfungo ni kusherekea na kumsahau mwenyezi mungu jambo ambalo si sawa.
Aidha Amewataka Kutambua kuwa Imani safi ni ile ya kuwatembelea watu wenye mahitaji,Wajane na Wagonjwa pamoja na malezi mazuri ya watoto.
Baadhi ya Wananchi na Wakristo mkoani Njombe akiwemo Richard Mguli na Alinani Baraka wamesema viongozi wa dini wanayo nafasi kubwa ya kuwaweka kwenye mstaari mnyoofu wananchi ili wasikengeuke kwani baadhi wachungaji na viongozi wengine wa dini hivi sasa wamekuwa wakijikita kwenye masuala ya miujiza na kutafuta fedha badala ya kuwaelekeza watu wamjue mungu.
Hata hivyo wanaweka wazi sababu za ukiukaji wa maadili,ujambazi,wizi na hata ubakaji kuwa husababishwa na malezi,Tamaa,Kudorora kwa uchumi na baadhi ya viongozi kutowajibika vitendo ambavyo vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara mkoani Njombe.
Baada ya mfungo wa siku 40 Wakristo duniani kote wanasherekea siku kuu ya Pasaka ya Ufufuo wa Bwana wetu Yesu Kristo.
0 Comments