Header Ads Widget

TAASISI YA MAOMBI, KUMWOMBEA RAIS SAMIA YAZINDULIWA RASMI MKOANI SIMIYU





Na Zurufa Halfan Matukio Daima Simiyu 


Taasisi ya maombi kwaajili ya kumuombea rais Samia suluhu hassan na wasaidizi wake imeanza maombi katika kipindi cha pasaka  na kuwasisitiza watanzania kuendelea kuilinda na  kudumisha amani ya Tanzania 


Msemaji Mkuu wa taasisi hiyo mchungaji Fabian Masaga ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa taasisi hiyo uliofanyika katika, kanisa La kiinjili La kilutheri Tanzania usharika wa ebeneza Nyashimo wilaya ya Busega na kuhudhuriwa na Waumini wa madhehebu mbalimbali na kusema maombi hayo yatafanyika nchi nzima na uzinduzi kitaifa unatarajia kufanyikamwezi Mei mwaka 2024 Mkoani Dodoma. 

Masaga amesema wameamua kuanzisha taasisi hiyo kama chombo maluum cha maombi, na kuwaomba Waumini kuwaombea viongozi wa taifa wakati wakifanya shughuli za kitaifa ili kuwatia nguvu 


Baadhi ya wachungaji wamesema ujio wa taasisi hiyo utasaidia viongozi za Chini kuongoza wananchi kwa hofu ya Mungu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI