Header Ads Widget

ASKOFU DR KIPANGULA :TUENDELEE KUOMBEA UCHAGUZI WA


ASKOFU wa kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mufindi Dkt Antony Kipangula ametaka Watanzania kuendelea kuomba Kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika mwaka huu pia kuombea maandalizi ya uchaguzi mkuu mwakani ili kupata Viongozi wenye hofu ya Mungu.

Akitoa Salamu za Pasaka Katika ushaurika wa kanisa kuu la Mafinga ,askofu Dkt Kipangula alisema suala la uchaguzi wa Serikali za mitaa ni muhimu Sana Katika Taifa hivyo lazima maandalizi yake yaendane na Maombi ili kupata Viongozi wenye hofu ya Mungu.

Alisema uchaguzi wa Serikali za mitaa ni uchaguzi utakaounda Serikali Kwa ngazi za vijiji na Mitaa hivyo iwapo watapatikana Viongozi wasio na sifa itakuwa mzigo Kwa Taifa .

"Lazima Viongozi wenye sifa wapatikane ili kuja kupata madiwani ,wabunge na Rais Mwenye hofu ya Mungu kwenye uchaguzi mkuu mwakani "

Pamoja na kutaka Watanzania Kwa Imani zao Kila mmoja kuendelea kuombea uchaguzi huo ,pia alitoa wito Kwa wale wenye sifa kujitokeza kugombea nafasi mbali mbali badala ya kuwa watazamaji na kuwaachia wale wasio na sifa .

Katika hatua nyingine askofu Dkt Kipangula amempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kuendelea kuchukizwa na vitendo vya ufisadi Katika Taifa .

Alisema Ripoti za CAG na Ile ya Takukuru ambazo Rais Dkt Samia amekabidhiwa ameonesha kuchukizwa na matumizi mabaya ya fedha za umma .

Hivyo alisema maagizo ya Rais Dkt Samia Kwa wale wanahusika na upotevu wa fedha za umma ni vema yakafanyiwa kazi ikiwa ni pamoja na wahusika kuchukuliwa hatua Kali.

Kuhusu vitendo vya ubunjifu wa amani vinavyoripotiwa kutokea Visiwani Zanzibar Kwa baadhi ya waamini wa dini kudaiwa Kupiga watu wasiofunga alitaka Serikali kuthibiti Hali hiyo kwani ni hatari Kwa ustawi wa Taifa na kutaka watu wasilazimishwe kufunga wakati Imani zao haziwaruhusu.

Alisema suala la kufunga ama kutofunga ni Imani ya mtu na Imani hailazimishwi hivyo ni vizuri watu kufundishwa Imani na wakielewa wafunge Kwa mapenzi yao ila si Kwa lazima .

Akielezea Kuhusu Dayosisi hiyo mpya ya Mufindi alisema Kwa Sasa kanisa linaendelea kupanga vema safu ya Viongozi watakaoongoza Kwa kipindi Cha miaka mitano.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI