Header Ads Widget

ZAHANATI YA MIAKA 90 YATELEKEZWA...

ZAHANATI ya Mashati wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro iliyojengwa zaidi ya miaka 90 iliyopita ipo hatarini kuanguka baada ya kuta za zahanati hiyo kuweka nyufa.

Kwa mujibu wa Diwani wa kata ya Katangara Mrere, Venance Mallel amesema kuwa toka zahanati hiyo ambayo inahudumia wananchi wa kata za Katangara Mrere na Kisare wilayani Rombo haijafanyiwa ukarabati muda mrefu huku majengo yake yakiwa yamechakaa. 

Alitumia nafasi hiyo kuiomba serikali kuikarabati zahanati hiyo ikiwemo upanuzi wa majengo ili kuendana na wakati wa sasa. 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI