Header Ads Widget

SERIKALI KUENDELEA NA TATHIMINI YA UJENZI WA BARABARA YA MABOGINI-KAHE.


NA WILLIUM PAUL, 

SERIKALI imedai inaendelea na tathimini kea ajili ya ujenzi wa barabara ya inayounganisha Mabogini-Kahe inayounganisha majimbo ya Moshi vijijini na Vunjo wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro. 


Hayo yamekuja baada ya Mbunge wa Jimbo la Moshi vijijini, Profesa Patrick Ndakidemi kuuliza swali la nyongeza kuwa Barabara ya Mabogini-Kahe inahudumia majimbo mawili ya Moshi vijijini na Vunjo ambapo barabara hiyo imeharibika sana kutokana na mvua za Elnino zinaziendelea je serikali inampango gani wa kukarabati barabara hiyo. 


Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Ofisi ya Rais na Serikali za mitaa Tamisemi Deogratius Ndejembe alisema kuwa, Serikali kupitia wakala wa barabara vijijini na mijini (Tarura) imeshapeleka milioni 368 katika halmashauri ya Moshi vijijini kwa ajili ya ukarabati wa barabara mbalimbali ikiwemo barabara ya sekondari ya Elimo na Muungano



Alisema kuwa, kuhusu barabara ya Mabogini-Kahe inayounganisha Jimbo la Moshi vijijini linaloongozwa na Prof. Patrick Ndakidemi na jimbo la Vunjo linaloongozwa na Dkt. Charles Kimei inaendelea kufanyiwa tathimini ili kujengwa. 

Mwisho.. 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI