Header Ads Widget

VIFAA VYA UJENZI WA SHULE YA WASICHANA YA MKOA TANGA VIHAKIKIWE NA TBS

Na Mbaruku Yusuph Matukio Daima APP, kilindi 

MWENYEKITI wa CCM Mkoa Tanga Rajabu Abdurahman ametoa maagizo kwa timu yake ya wataalamu kuhakikisha vifaa vya ujenzi wa shule ya Sekondari ya wasichana ya Mkoa Tanga yenye thamani ya Sh bil 3 vihakikiwe na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ili kujiridhisha na ubora unaotakiwa.


Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa Tanga Rajabu Abdurahman wakati wa uzinduzi wa sherehe za miaka 47 ya kuzaliwa kwa CCM Mkoani hapa ambapo uzinduzi huo ulikwenda sambamba na upandaji wa miti 500 katika shule hiyo ambayo inajengwa katika kata ya Mabalanga Wilaya ya Kilindi Mkoani Tanga. 

Komred Rajabu alisema lengo la uhakiki huo ni kuepuka udanganyifu unaoweza kufanywa kama ulivyofanyika katika miradi mingine jambo ambalo halitakiwi kujirudia tena hasa katika miradi mkubwa kama hiyo.


"Matukio ya udanganyifu wa vifaa ulishawahi kutokea katika Wilaya ya Handeni na hata kilindi lakini baada ya Chama na Serikali kufuatilia tulibaini udanganyifu wa ubora wa mabati na tulichukua hatua,sitarajii kwenye mradi mkubwa kama huu yatokee mambo kama hayo"Alisema Rajabu.

"Tumekagua faili na tumebaini hakuna ramani wala BOQ na nimeagiza wasimamizi wa mradi huo watuletee vielelezo na muongozo wa mradi huo ili timu yangu mbali ya kuchukua kipande chanbati kwa ajili ya kwenda kupima ubora wake TBD,lengo letu ni kujiridhisha na ubora wa vifaa vinavyotumiwa katika mradi huo ?Alisema Komredi Rajabu. 


maadhimisho hayo yameanzia katika ukaguzi wa ujenzi wa mradi wa shule hiyo ambao ilikuwa ni hadithi ya muda mrefu kutokana na mvutano wa Wilaya za Handeni na Kilindi wapi shule hiyo itajengwa jambo lililopelekea fedha hizo Bil 3 kurudishwa Serikalini.


"Tumeoambana kama chama kwa kushirikiana na Serikali fedha hizi zikarudishwa na hatimae mradi unakwenda vizuri na ni wajibu wetu kuusimamia mradi huu "Alisema Rajabu. 


Hata hivyo Mwenyekiti huyo alisema wananchi watambue Rais Samia anapambana kutafuta fedha kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu hivyo ni wajaibu kwa watendaji wa Serikali na Viongozi wa Chama kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa wakati na iendane na thamani halisi iliyotengwa.

Mkuu wa Shule Mama Wilayani Kilindi Selestina Kavishe alikiri kuwa May 5/2023 Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi ilipokea Shs Bil 3 kwa ajili ya kugharamia ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika shule hiyo ungawa zipo changamoto zilizojitokeza na kupelekea mradi huo kutikumalizika kwa wakati.


Mwalimu Kavishe ambae alimuakilisha Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Kilindi alizitaja changamoto hizo ambapo ni pamoja na kunyesha kwa mvua kubwa,ukosefu wa maji eneo la mradi,kusumbua kwa mfumo wa malipo,eneo la ujenzi kutoendana na ramani na kukisekana kwa umeme eneo la mradi.


alisema changamoto zote hizo zilitafutiwa ufumbuzi na mamlaka husika na mradi unaendelea huku matarajio ya shule hiyo kukamilika mwezi wa pili mwaka huu wa 2024.


Hata hivyo alisema shule hiyo itakuwa na madarasa 12,mabweni 8,jengo la utawaka 1,chumba cha waginjwa 1,nyumba za walimu 2,bwalo la chakula 1,jengo la jenereta 1,jengo la vyoo vya wanafunzi matundu 16,maabara za kemia na bailojia 2 na maabara za fizikia na jiografia 2

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI