NA HERRIET MOLLA ,MBEYA
KAMISAA wa sensa Nchini na spika mstaafu wa bunge la Tanzania, Anne Makinda, amepongeza waandishi wa habari, kwa ushiriki wao wa kutoka habari zenye kuhamasisha wananchi umuhimu wa wa sensa ya watu na makazi kwanzia hatua ya kwanza.
Akizungumza na waandishi wa habari kutoka mikoa ya Iringa, Mbeya na Songwe katika mafunzo ya usambazaji na matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022, amesema mafunzo hayo yatakuza uelewa wa uandishi wa habari za takwimu.
Pia amewakumbusha waandishi wa habari kuandika habari zenye takwimu sahihi kwa kuzingatia sheria na vyanzo halisi ili kujilinda wenyewe.
Akifungua mafunzo hayo, mkuu wa wilaya Mbeya Beno Malisa, amewataka waandishi wa habari kuibua mada na mijadala mbalimbali yenye faida zinazo husisha matokeo ya sensa ya watu na makazi ili kutoa uelewa mpana kwa wananchi.
DC Malisa, amesema matokeo hayo, yakitumika vizuri yataleta maendeleo makubwa kwa Watanzania.
0 Comments