NA RAYMOND MINJA ARUMERU
WANANCHI wa kijiji cha Makiba kata ya Makiba Kitongoji cha Songa mbele wamemuangukia Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuwasaidia kutatua changamoto ya barabara inayoelekea kwenye kituo hicho cha afya kwani wakina mama wengi wemekuwa wakijifungua njiani kutokana na ubovu wa barabara kuelekea kwenye kituo hicho
Kamera yetu ya Matukio Daima Media ilipita katika eneo hilo na kukuta wanachi wakitumia majembe na na sururu kufukia mashimo hayo ili kuweza kusaidia kupunguza changamoto hiyo
akizungumza katika eneo la tukio mwemyekiti wa kijiji hicho Lemomo Kishali alisema eneo hilo limekuwa ni shida sana kupitika hasa kipindi cha mvua kueleakea kwenye kituo hicho cha meta kinachobudumia wakazi wengi kutoka kata mbalimbali katika eneo hilo
" kwakeli sisi huwa tunapata shida sana katika eneo hili kuna madibwi makubwa na ikifika kipindi cha mvua hapa hapapitiki na hii ndio njia ya kwenda hapo kituo cha afya kwa hiyo mars nyingine wamama wanajifungulia njiani hapa kwenye madibwi ya maji
Lemomo anasema kuwa baada ya kuona changamoto ni.kubwa ndipo alipoamua kupiga pembe ili kuwaomba wananchi waweze kusaidia kutoa nguvu kazi ili kujaribu kuziba mashimo hayo
"Moja wa waendesha pikipiki eneo hilo alisema wamekuwa wakipata shida sana kipita eneo hilo kwani kumekuwa na tope jingi na maji jambo ambalo linawafanya washindwe kupita.
kuukweli huku tumesahaulija mana hii barabara ni shida mana ukitazama haya madibwi ni hatua chache tu kufika kituo cha afya kwa meta ila huwezi kufika mana madibwi makubwa na maji mengi hivyo hembu watusaidie mana nishida hapa tuna diwani ,tuna mbunge ila hakuna kitu shida tupu"
kwa upande wake Mariamu Ndalimu anasema barabara hiyo imekuwa ni changamoto kubwa hasa kwa wamama wanaekwenda kwenye kitio hicho cha afya cha Meta Makiba.
"kiukwe wanawake wajawazito wanapata shida sana kwenda kituo cha afya kutokana na ubovu wa barabara wamama wanajifungulia njiani kabla ya kufika kituo cha afya,na wakati mwingine hata mama mjamzito akipata shida kwenye kituo hicho ambulence zikija zinashindwa kupita kwenda kumchukua ndio mana hata mimi leo nimekuja kuziba haya mashimo kwakweli tunateseka"
Kwa upande wake katibu wa tawi wa Chama cha Mapinduzi CCM Daud Mangole amesema barabara hiyo imekuwa ni changamoto kubwa na wamekuwa wakipata malalamiko mengi kutoka kwa wananchi na kwa badhi ya wamama kujifungulia njiani
"Kwa kwelii hii barabara ni shida na siso kama chama tumepata malalamiko mengi jishi wamama wavavyo pata shida hapa kwenda kujifungua ndio mana hata mimi niko hapa leo kusaidiana na watu wangu kuziba haya mashimo."
Hata hivyo Mandole inaiomba Tarura kuweza kufika kwenye eneo hilo na kutatua changamoto hiyo kwani kwa nguvu za wananchi hawawezi kulimaliza tatizo hilo.
0 Comments