![]() |
Mwenyekiti wa ACT Wazalendo mkoa kigoma Kiza Mayeye (katikati) akiwa na viongozi wenzake walioshinda uchaguzi Katibu wa mkoa Yunus Ruhonvya (kushoto) na Katibu Mwenezi Azizi Ally ( kulia) |
Na Fadhili Abdallah,Kigoma
WAJUMBE wa mkutano mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo mkoa Kigoma kwa kauli moja wamemchagua Kiza Mayeye kuwa Mwenyekiti wa mkoa wa chama hicho kwa miaka mitano ijayo.
Mwenyekiti wa ACT Wazalendo mkoa Kigoma aliyemaliza muda wake, Sendwe Ibrahim ambaye alitechaguliwa na wajumbe kuongoza mkutano huo wa uchaguzi alisema juwa Mayeye aluchaguliwa kwa kupata kura 108 kati ya kura 134 za wajumbe wa mkutano huo.
Katika matokeo hayo Mayeye aliwashinda wapinzani wake Nicholous Cosmas aliyepata kura 24 na Bailel Manwa aliyepata kura mbili.
![]() |
Kiza Mayeye Mwenyekiti w ACT Wazalendo mkoa Kigoma |
Aidha Mwenyekiti huyo wa uchaguzi huo alimtangaza Yunus Ruhonvya kuwa Katibu wa mkoa akipata kura 65 akimshinda mshindani wake Frank Ruhasha aliyepata kura 64.
Nafasi ya Katibu Mwenezi ilichukuliwa na Azizi Ally aliyepata kura 55 akimshinda Kalembe Masoud aliyepata kura 51 na Ibrahim Feruzi aliyepata kura 25 huku Tatu Amani akiibuka kuwa Mwenyekiti wa ngome ya wanawake kwa kupata kura 14 akimshinda Isabela Kabululu aliyepata kura mbili.
Aidha Mwenyekiti huyo wa uchaguzi alimtangaza Selemani Simba kuwa mwenyekiti wa ngome ya wazee na Athumani Nyamitwe kuwa Katibu wa ngome hiyo.
katika ngome ya vijana mkoa wajumbe walimchagua Hamza Abdallah kuwa Mwenyekiti na Uledi Amri Rajabu kuwa katibu wa mkoa ngome ya vijana.
![]() |
Wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi mkoa Kigoma |
0 Comments