Header Ads Widget

MASHINDANO YA KUIMBA NYIMBO KUPINGA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA

Mamlaka ya Kuthibiti na kupambana na madawa ya Kulevya DCEA Kanda ya Pwani imefanya Mashindano ya kuimba nyimbo za kupinga Matumizi ya Dawa za kulevya yenye lengo la Kutoa elimu kwa Wananchi kupitia sanaa

Mashindano hayo yamefanyika Katika uwanja wa Shule ya Msingi Mnazi mmoja, Kata ya Mingoyo Manispaa ya Lindi ambapo awali akizungumza kuhusu madhumuni ya Mashindao hayo Kaimu kamishna wa Kanda ya Kusini Bi.Salome Mbonile amesema wanatoa elimu kwa watu wote huku akisema wamechagua eneo hilo kwa kua ni makutano ya barabara za wilayani na mikoa ya jirani.

Naye Mgeni rasmi wa Mashindano hayo Afisa utamaduni Mkoa wa Lindi Mkalage Nkinda  ametoa pongezi kwa Mamlaka ya Kuthibiti na kupambana na madawa ya Kulevya kwa kutumia Sanaa kwenye kuendelea kutoa elimu na kuwasihi wasanii kutumia vizuri majina yao pasi na kujiingiza kwenye makundi hatarishi.

Kwa upande wao baadhi ya wasanii walioshinda Kwenye Shindano hilo  akiwepo Dox Kamanda pamoja na Nasoz wamewasihi vijana wenzao kutojihusisha na matumizi ya madawa huku wakiahidi kutumia Sanaa yao kutoa elimu kwa jamii


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI