Nyumba zaidi ya 300 ikiwemo ofisi ya Serikali ya mtaa, zilizopo kwenye hifadhi ya barabara, zinatarajiwa kubomolewa katika mitaa mitatu ya Kata ya Chanika, wilayani Ilala jijini Dar es Salaam huku wananchi wakilalamika kutojua hatima ya fidia zao.
Barabara hiyo ya Chanika-Mbande na Pugu- Chanika, mitaa inayotarajiwa kukumbwa na bomoabomoa hiyo ni Lubakaya, Lukooni na Zingiziwa.
Tayari baadhi ya nyumba zimewekewa alama ya X na kuandikwa bomoa ikiwamo ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Lukooni, ambayo viongozi wake hawakuwa tayari kuzungumza.
Bomoabomoa hiyo, imethibitishwa na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) kupitia meneja wa wakala huo Dar es Salaam, John Nkumbo.
Amesema hiyo ni shughuli endelevu ambayo wamekuwa wakiifanya katika kulinda hifadhi za barabara zao.
CHANZO:Mwananchi
0 Comments