KITUO cha kuendeleza vipaji African Talent Forum-TZ (ATFT) kimewataka wadau wa sanaa kuwekeza kwa wasanii ili kutoa ajira kupitia sanaa.
Akizungumza kwenye kikao maalumu kujadili masuala mbalimbali ya namna ya wasanii wanavyoweza kupata fursa za kuinua vipaji vyao Mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho Rosemary Bujash amesema kuwa vipaji hivyo bila ya kuendelezwa havitaweza kufika mbali na kufikia lengo la kutoa ajira kama ilivyo kwa wasanii wakubwa nchini.
Kwa upande wake ofisa utamaduni wa Halmashauri ya Mji Kibaha Evarista Kisaka amesema kuwa moja ya changamoto kwa wasanii wachanga ni kutojitangaza hivyo kituo hicho wakitumie ili kutangaza kazi zao.
Naye mwenyekiti wa Wasanii Kibaha Jumanne Kambi amesema kuwa wasanii wako wengi lakini hawapati fursa kuonyesha vipaji vyao hivyo watashirikiana na kituo hicho kuinua wasanii.
Awali Ofisa Maendeleo ya Jamii Kata ya Mkuza Victoria Andrea amesema kuwa wasanii wanapaswa kuwa wabunifu ili kuboresha kazi zao ziweze kuvutia watu.
0 Comments