Header Ads Widget

WAHITIMU WAWALILIA WADAU KUKICHANGIA KITUO CHAO ILI KUWA BORA ZAIDI

Na Shemsa Mussa,Kagera. 

Wahitimu wa elimu ya awali katika kituo cha kulea watoto wadogo cha Gift Education Centre  kilichopo kata kibeta mtaa wa Omukituli  Manispaa ya Bukoba wamewaomba wadau kukichangia kituo hicho ili kuwa bora zaidi 


Akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wote Ndg Robert Van  Robertson amesema licha ya walimu kufanya jitihada nzuri za ufundishaji bado kituo hicho kinakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo Vifaa vya Michezo, Mikeka kwa ajili ya kukalia,Chumba cha darasa pamoja na Vifaa kwa ajili ya kufundishia na kusema kuwa endapo changamoto hizo zitatatuliwa itakuwa ni hatua kubwa kwao.


Aidha amesema kituo hicho kilianzishwa mwaka 2021 kikiwa na wanafunzi 3 pamoja na chumba kimoja cha darasa na mpaka sasa wapo jumla ya wanafunzi 50 ikiwa wavulana ni 20 na wasichana 30 huku walimu wakiwa 2  wote wa kike



Ndg Robert  ameongeza kuwa jumla ya wahitimu wanaomaliza elimu ya awali  mwaka  2023 ni 20 huku wakiwa wanajivunia kuhitimu wakiwa wanajua kusoma na kuandika huku akisema jitihada zote hizo ni ushirikiano wa walimu na wazazi.


Akiongea kwa niaba ya wazazi Bi Hope Alibalio ambaye pia mi mlezi wa watoto  watatu wanaohitimu katika kituo hicho amesema anakishukuru kituo hicho kwa kuwalea na kuwafunza wajukuu zake na   kwa usimamizi  mzuri unaongozwa na mkuu wa kituo hicho cha Gift Education Centre.


Nae Mkuu wa kituo cha  Gift Education Centre  Bi Careen Christom amewashukuru wazazi kwa kuendelea kumuamini na kumpatia watoto na amewaomba wazazi wote wenye watoto umri wa kuanza awali  kuwapeleka kituoni kwake kwani watapata matoke mazuri kwa muda mchache.


Pia nae Bw Chrizostom Paulo Lugalabamu  ambaye alikuwa mgeni rasmi amesema ni vema kuendeleza ushirikiano baina ya wazazi na walimu ili kushirikiana katika malezi na makuzi ya mtoto na kusema kuwa bado watoto hao ni wadogo wanahitaji kushirikiana pia ameahidi kutoa atakachajaaliwa na Mungu ili kupunguza changamoto zilizopo kituoni hapo.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI