Header Ads Widget

VYUO VYA KATI NJOMBE VYAOMBA MKOPO KWENYE KOZI ZOTE

 


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Wakati serikali ikianza kutoa  mikopo Kwa elimu ya Kati kwenye baadhi ya Kozi za kipaumbele zikiwemo za afya na Kilimo,Wanafunzi wa vyuo vya Kati mkoani Njombe wameomba kozi zote kupata mkopo hususani Kwa wanafunzi wanaotoka katika familia duni.



Rais wa serikali ya wanafunzi wa Chuo Cha Aman College kilichopo chini ya kanisa la KKKT Dayosisi ya kusini Njombe John Mbawala   katika mahafali ya 12 Kwa niaba ya wanachuo hao amesema Kuna baadhi ya wanavyuo wanaotoka kwenye familia duni wanashindwa kusoma Kwa kukosa mkopo Jambo linalokatiza ndoto zao.


Kauli hiyo inaungwa mkono na baadhi ya wahitimu wa chuo hicho akiwemo Maria Mtuta na Recho Kiula  ambao wanasema baadhi yao wameshindwa kuhitimu kwa sababu ya kukosa fedha jambo ambalo serikali inapaswa kuingilia kati.


Mkuu wa Chuo Cha Aman Mchungaji  Dokta Johnson Gudaga amesema wamelazimika kurejesha kozi zilizoondolewa awali kutokana na maombi ya watu Wengi Jambo linalochagiza kuwapo Kwa mwamko mkubwa wa elimu mkoani Njombe.


Katika mahafali Hayo mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe Claudia Kitta Kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Njombe anasema utaalamu waliosomea unapaswa uwasaidie kukabiliana na wimbi la ukosefu wa Ajira badala ya kulalamika.


Askofu wa KKKT Dayosisi ya kusini Njombe George Mark Fihavango akiwa na mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe Mhe. Claudia Kitta

Mwenyekiti wa bodi ya chuo hicho Dokta  Egidio Chaula  amesema Suala la maadili na ukombozi wa kifikra ndio nguzo pekee zinazoweza kuwakomboa watanzania


Jumla ya wahitimu 120 wa kozi za Maendeleo ya Jamii,Tehama na usimamizi wa biashara wamehitimu masomo na kusherekea kwa mahafali ya 12 tangu kuanza kwa chuo hicho cha elimu ya kati mkoani Njombe.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI