Matukio Daima APP, Mtwara,
Kutokana na tatizo la ajira nchini wanafunzi zaidi ya 436 wa chuo cha uhasibu tawi la Mtwara wampata mafunzo ya ujasiriamali yatakayo wawezesha kuzichangamkia fursa mbalimbali.
Akizungumza katika mafunzo hayo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Tanzania William Pallangyo amesema kuwa ili kukabiliana na soko la ajira nchini wamebuni njia ya kuwezesha wanachuo ili waweze kujiajiri wenyewe.
Amesema kuwa zaidi ya wanachuo 26,000 wanaosoma katika chuo hicho nchi nzima hivyo utolewaji wa elimu hiyo utawezesha wao kujiajiri wenyewe.
“Wapo ambao hawataweza kuajiriwa hivyo wataweza kujiajiri wenyewe hatua ambayo itaongeza hamasa kwa wengine pia tunao wanafunzi 26,000 nchini nzima wapo watakao jiajiri ndio maana tunawafundisha leo na kuwaandaa ili wajiajiri wenyewe” amesema Pallangyo
Nae Agatha Kelvin mwanafunzi wa chuo hicho amesema kuwa wamenufaika na mafunzo ikiwemo namna bora ya kuzitambua fursa mbalimbali zilizo katika mazingira yao zitakazowasaidia kujiajiri.
Amesema kuwa katika chuo hicho ameweza kubuni mradi wa kuongeza thamani katika mnyororo wa zao la korosho kwakutengneneza vitu mbalimbali.
“Mimi nna mradi wa korosho ambao nitauza kwa njia ya mtandao ambapo ninatengeneza unga, peanut na biscuit za korosho ambapo watu wengi wanataka korosho zenye viwango ambapo sisi tutaongeza thamani kwenye bidhaa hii iweze kuwafikia wengi mahali mbalimbali nchini”
“Tunatarajia kuuza kwa njia ya mtandao ambao tutasafirisha kwenda katika nchi mbalimbali na wengine wa rejareja nao pia tutawasafirishia”
"Unajua wengi wanauwezo mkubwa wa kuziona fursa lakini wakielimishwa wanaongeza ujuzi zaidi ndio maana sisi tunaona ipo fursa kubwa kwenye zao la korosho ndio maana nimeingia kwenye tasnia hiyo naamini itanipa mwangaza kujiajiri na kuajiri”
Nae Hellen Maliki mwanafunzi wa TIA amesema kuwa baada ya kupata mafunzo ya ujasiliamali ambebaini kuwa watu weye ulemavu wana majhitaji mengi na wakati mwingine hawezi kuyafikia hvyo kupitia mtandao atawafikia na kutoa elimu kwa.
“Mimi nimekuja na mradi wa kusaidia watu wenye ulemavu ambao utaunganisha kwa kuwafikia ili waweze kushiriki katika uchumi wanchi ambapo tutawawezesha na kuwaonyesha ujasiriamali wao na bidhaa kupitia mtandao wetu” amesema Maliki
0 Comments