Header Ads Widget

RC IRINGA APONGEZA ATAPE CTF -MINI -RETREAT,ATAKA VIJANA KUTOCHAGUA KAZI

 

Na Hamida Ramadhan,Matukio Daima App 

MKUU wa Mkoa Iringa Halima Dendego ameiasa jamii na hasa Vijana kuacha tabia ya kuchagua kazi na badala yake wajikite katika kufanya kazi yoyote ya halali na yenye manufaa na tija kwako.


Ameyasema hayo mjini Iringa katika wakati akifungua  Mkutano wa TAPEA CTF -MINI -RETREAT IRINGA 2023 mkutano uliwakutanisha waumini  wa kanisa la Sabato ambao ni wajasiliamali na wafanyabiashara kutoka mikoa ya Dodoma Kiteto na Iringa huku ikiendeshwa kwa kauli mbiu isemayo " SHINDA VIKWAZO.


MKUU huyo ameendelea kuitaka jamii kuacha kelele na kulialia vikwazo kwa mwanadamu ni lazima lakini wakumbuke kuwa  wakifanya jitihada katika kupambania ndoto zao na kumuweka Mungu mbele na mafanikio watayaona .


Amesema ili kusonga mbele ni lazima Kijana awe mbunifu kichwani ,kuwa na hofu ya Mungu na mfukonikuwepo na kitu kwani katika jamii yetu walioendelea ndio wanaomjua Mungu mtu akiwa na njaa na Hata Mungu anamsahau hivyo semina au mkutano huu umekuja Wakati sahihi kuwaondolea vikwazo na hofu jamii na kuchapa kazi.




"Hata Mimi Mkuu wamkoa wenu ninavikwazo pia Ila kimbilio langu kubwa ni kwa Mungu wangu ukisema ukiomba kwa thati na nia thabiti unajibiwa kwa Wakati kwani Mungu hujibu kwa wakati na kumpitisha mtu pale pasipopitika," amesema Mkuu huyo .


Na kuongeza" Mungu akikupa jaribu lolote usinung'unike badala yake pigagoti muombe Mungu Sana majibu utayaona,lakini pia nimefarijika mkutano huu kufanyika Mkoani Iringa kwani ni ukweli kwamba Iringa ipo salama na uchapaji kazi ndio Silaa yetu na tunafursa nyingi za uwekezaji ," amesema Mkuu huyo.




Katika hatua nyingine amemshukuru na kumpongeza Rais wa awamu ya sita Dkt,Samia Suluhu Hassani kutokana na miradi mingi ya kimkakati na maendele ilipo hadi pempezoni.


"Tumuombee Rais wetu na tukemee wale wote wanaobeza mazuri anayofanya mama yetu," amesema 



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI