Header Ads Widget

MASHUJAA YACHOMOZA AZAM FEDERATION CUP

  




Na Fadhili Abdallah,Kigoma

 

TIMU ya soka ya ligi kuu ya Mashujaa ya mkoani Kigoma imeyaanza vizuri mashindano ya kombe la shirikisho la Azam baada ya kuichapa timu ya Mbuga FC ya mkoani Mtwara kwa mabao 3-2.

 

Katika mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa Lake Tanganyika Mjini Kigoma wageni hao kutoka Mtwara ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa kwenye dakika ya nane ya kipindi cha kwanza kupitia kwa mchezaji wake Haridi Ramsachi kufuatia pasi ya Fadhili Waziri.

 

Mbuga FC ambao ni mabingwa wa soka mkoa Mtwara walionekana kutawala mchezo huo kwa kipindi chote cha dakika 45 za kipindi cha kwanza na hadi timu hizo zinakwenda mapumziko Mbuga FC ilikuwa mbele kwa goloi 1-0.

 

Timu ya Mashujaa ilianza kipindi cha pili kwa kasi na dakika ya kwanza ya kipindi cha pili (dakika 46) walipata goli la kusawazisha lililofungwa na Kelegea Wazanga akimalizia pasi ya Athuman Makambo.

 

Kufuatia kuingia kwa goli hilo timu ya Mbuga FC iliongeza mashambulizi langoni mwa Mashujaa na kupata goli la pili lililofungwa na Azizi Chikoyo kwa kiwachwa kufuatia krosi iliyopigwa kwenye goli la mashujaa na kumshinda golikipa Hashim Mussa wa Mashujaa.

 

Kufungwa kwa goli la pili la Mbuga FC kuliwafanya Mashujaa kufanya mabadiliko ya wachezaji wake mabadiliko yaliyozaa matunda kwenye dakika ya 54 kwa goli la penati lililofungwa na Ismail Mhesa aliyeangushwa ndani ya eneo la penati na mchezaji wa Mbuga FC Haridi Ramsachi.

 

Mabadiliko hayo ya wachezaji yaliongeza nguvu kwa timu ya Mashujaa na kufanya mashambulizi langoni mwa Mbuga FC ambapo dakika 65 Masome Mashauri aliipatia Mashujaa goli la tatu akimalizia pasi ya Ismail Mhesa ambapo hadi kipyenga cha mwisho kinapulizwa Mashujaa ilikuwa mbele kwa goli 3-2.

 

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI