Mkutano Mkuu wa CCM Jimbo la Mufindi Kusini kwa kauli Moja imeadhimia Kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Utekelezaji mzuri wa Ilani ya CCM katika wilaya ya Mufindi.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu maalum mbele ya Mgeni Rasmi Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Ndg. Issa Gavu wameadhimia kwa kauli Moja kumchangia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Fomu ya kugombea Urais Mwaka 2025 - 2030.
Dhumuni ni kuwaongoza tena na kuthibitisha uongozi wake kuwa hauna mashaka katika kuwatumikia watanzania hasa jimbo la Mufindi kusini.
Aidha Mkutano Mkuu wa jimbo la Mufindi Unaelekeza watendaji wa serikali katika idara mbali mbali kutekeleza kwa wakati na ufanisi mkubwa Miradi ya Maendeleo katik Jimbo la Mufundi Kusini.
Mjumbe wa halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndg. Issa Gavu amepokea Michango ya kila mjumbe na kila kata katika jimbo la Mufindi Kusini na kukamilisha Jumla ya Tsh. Milioni mbili laki mbili arobaini na Saba mia saba hamsini, (Tsh 2,247,750) za kumchukulia Fomu Ndg . Samia Suluhu Hassan Mgombea Urais 2025 - 2030 kupitia tiketi ya CCM .
Ndg Issa gavu amemaliza kwa kuwashukuru wajumbe kwa Imani kubwa waliyonayo kwa mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg. Dkt. Samia Suluhu Hassan ,
“Fedha hizi nimepokea na nitazifikisha kwa Mhusika naombeni mwendelee kuwa na imani na viongozi wa Chama na serikali kama mlivyoonyesh Imani kwa kiongozi wetu wa Nchi”. Amesema Ndg. Issa Gavu
0 Comments