Na Shemsa Mussa,Kagera
JESHI la polisi Mkoa Kagera limefanikiwa kuwakamata watu watatu wakituhumiwa kushiriki mauaji ya watoto saba wa familia moja katika kijiji cha nyakanazi wilaya ya biharamlo Mkoani Kagera .
Akitoa taarifa ya kukamatwa kwa watu hao mbele ya waandishi wa habari kamanda wa polisi Mkoa Kagera Blasius Z Chatanda amesema kuwa tukio hilo la mauaji lilitokea tarehe 13 Novemba Mwaka huu na watu hao walikamatwa wakiwa wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita walipokimbilia baada ya kutekeleza mauaji ya watoto hao wa Mzee Lazaro Sanabanka Mwenye umri wa miaka 61 mkazi wa kijiji Nyakanazi.
Kamanda chatanda, amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Jenipher Petro Nyakidi mwenye umri wa miaka 19 mkazi wa Nyakanazi ,Mernes Petro mwenye umri wa miaka 22 mkazi wa Nyakanazi ,Emmanuel Julius Noel mwenye umri 31 mkazi wa Masumbwe.
Kamanda ameeleza kuwa baada ya kuwakamata watuhumiwa walihojiwa na kukiri kuhusika katika mauaji hayo baada ya kuweka sumu ya kuuwa wadudu katika mboga za majani ya Maharage kwa lengo la kulipiza kisasi katika familia ya mzee huyo kwa tuhuma za watoto wake kuiba kuku wao jogoo.
Amewataja pia waliofariki dunia baada ya kutumia mboga hiyo iliyowekewa sumu Melisa Lazaro mwenye umri miaka 11,Melinas mwenye umri miaka 9, Kahindi Samson mwenye umri miaka 9, Happynes Lazaro mwenye umri maika 12 BrianEzekiel miaka 3, Josephina miaka 5 na Meleciana Lazaro miaka 11 wote wakiwa wa familia moja ya mzee huyo.
Chatanda amesema kuwa jeshi la polisi litawafikisha Mahakamani watuhumiwa wote kwa mujibu wa sheria kwa nia ya kuwatia hatiani kli waweze kuadhibiwa na kusema kuwa iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia ya kutenda vitendo vya kikatili.
Aidha ametoa onyo kwa watu wote watakaothubutu kushiriki vitendo vya uhalifu yakiwemo mauaji kwani jeshi hilo litawachukulia hatua watakaobainika kufanya matukio yotote ya kiuharifu,huku akiwatakiwa wananchi kheri za sikukuu ya Christmas na Mwaka mpya wa 2024.
0 Comments