Header Ads Widget

ZITTO KUJENGA MIUNDO MBINU SOKO KUU KIBONDO

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe akizungumza na wajasiliamali wa soko la Samaki Kibondo akiwa kwenye ziara ya mikutano yake kwenye wilaya hiyo
Sehemu ya mazingira ya soko la samaki Kibondo likiwa na miundo mbinu duni ambayo inalalamikiwa na wajasiliamali ambapo kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe ameahidi kuiboresha

Na Fadhili Abdallah,kigoma

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amesema kuwa atatafuta wafadhili kwa ajili ya kufanya maboresho kwenye soko la samaki la wilaya ya Kibondo ambalo ni sehemu kuu ya soko la wilaya hiyo kutokana na miundo mbinu ya soko inayoleta changamoto kubwa kwa wajasiliamali kufanya biashara kwa tija.

 

Akizungumza na wajasiliamali na wafayabiashara wa soko hilo Zitto kabwe alisema kuwa anachukua hatua hiyo kuboresha soko hilo ambalo litasaidia kuwafanya wajasiliamali hao kufanya biashara zao kwa tija tofauti na sasa ambapo wamekuwa wakifanya shughuli zao kwa mashaka makubwa.

 

Zitto alisema kuwa kufanya biashara kwa mashaka kunatoa nafasi finyu kwa wajasiliamali hao kuchukua mikopo kwa ajili ya kuboresha na kupanua biashara zao kwani hawana uhakika na mahali wanapofanyia biashara hizo kama wanaweza kuendelea kuwepo kwa muda mrefu.

 

“Serikali inakusanya ushuru kila siku kwa wajasiliamali hao lakini mazingira yao ni mabovu sana wakati wa mvua hali ni tete sana maji yanapita katikati ya biashara zao huku kukiwa na matope kila mahali hivyo hakuna tija ya biashara wala tija katika kuimarisha uchumi wa watu hao, ACT kupitia kwangu lazima tufanye kitu kuwasaidia watu hao ili kuboresha mazingira haya ya kufanyia biashara,”Alisema Zitto Kabwe.

 

Awali wajasiliamali hao walimweleza kiongozi huyo wa Chama cha ACT Wazalendo kuwa wamekuwa wakifanya biashara kwenye mazingita magumu kutokana na kutokuwepo kwa paa wala mazingira mazuri ya kufanyia biashara ambapo wakati wa mvua inabidi kufunga biashara na kuzirudisha nyumbani.

 

Mmoja wa wajasiliamali hao, Joseph Masunzu alisema kuwa wanashindwa hata kuchukua mikopo kutoka sehemu mbalimbali kwa sababu hawana uhakika kama wataweza kuirudisha kwani maeneo wanayofanyia shughuli zao ni za mashaka na hawawezi kusema kama wataendelea kuwepo ama la.

 

Akizungumzia changamoto hiyo Afisa mipango wa halmashauri ya wilaya Kibondo, Adam Mapunda alikiri kuwepo kwa miundo mbinu duni ya soko hilo ambalo awali lilikuwa eneo la wazi na sasa wamebadilisha matumizi sambamba na kuwa na mpango wa kutenga fedha kenye bajeti ijayo ili kulifanyia maboresho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI