Header Ads Widget

RC MTWARA AZINDUA MSIMU WA KILIMO

Mtwara, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanal Ahmed Abbas amewaagiza viongozi na maafisa ugani kuhakiikisha kuwa mbegu za ufuta tani 10 zilizotolewa kwa wakulima na taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania Tari kituo cha Naliendele zinagawiwa kwa wakulima walioandaa mashamba pekee.


Akizungumza katika Uzinduzi wa maandalizi ya msimu wa Kilimo ambao umefanyika Nov 17, 2023 katika Kijiji Cha Nanyumbu, Halmashauri ya Wilaya Nanyumbu Mkoani Mtwara, sanjari na Uzinduzi wa Kilimo Cha Pamoja (Block Farming), Ugawaji wa mbegu za Ufuta na Mbaazi, Kuzindua Matumizi ya kipima udongo (Soil Scanner), amesema kuwa wakulima  walioandaa mashamba wapewe kipaumbele katika mgao wa mbegu hizo.


Amesema kuwa mkoa umejipanga kuongeza uzalisha na kulima kwa tija mazao ya korosho, mbaazi, ufuta, karanga choroko ambapo baada ya malipo wakulima mfanye maenedeleo na kubadilisha maisha yenu.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imedhamiria kuinua maisha ya Wananchi wake kupitia sekta Mbalimbali za kijamii na Uchumi ikiwemo Kilimo na hivyo katka msimu uliopita Serikali ilitoa ruzuku za pembejeo katika zao la korosho ambapo kwa Halmashauri za Mkoa wa Mtwara zilipokea viuatilifu Tani 21,048 za Salfa na viuatilifu vya Maji lita Tani Milioni Moja kwaajili ya kudhibiti magonjwa na wadudu wa zao la korosho. Ameongeza kuwa kwa msimu huu wa Kilimo. Serikali imetoa kilo 10,500 za mbegu za Ufuta aina ya Lindi 2002 ambazo amezikabidhi kwa mkulima mmoja Kama uwakilishi Lakini mbegu hizo zitagawiwa kwa Wakulima wengi zaidi ambao wapo tayari kufuata kanuni Bora za kilimo, taratibu na masharti ya Kilimo

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania Joseph Nzunda amesema kuwa taasisi hiyo kwakutambua mchango wa wakulima wa zao la ufuta watoa tani 10 za mbegu.


“Sisi tunafanya utafiti kwa mazao mbalimbali ili kuhakikisha kuwa wakulima wanapata mbegu bora  tunalima mbaazi hekali 800 na hekali 500 za ufuta na utmetenga zaidi ya tani 10 za uufta kwa mkoa ambapo tutaongeza kasi ya kuongeza uzalishaji”


“Wanunuzi wanangalia suala la kiafya ambapo wamehimiza tuwasisitize wakulima wetu nchini wengine wanahifadhi na dawa hivyo kupoteza ubora kaeni mbali na dawa  wengine wnaaweka taka taka bila kuangalia usafi”


“Ukipanda na ukapalilia mapema ndani ya wiki mbili  kisha utapunguzia mimea mstari kwa mstari sentimeta 50 na mmea hadi mmea sentimeta 10 kama mbolea haitoshi weka mbolea ya kupandia baada ya wiki 3 weka mbolea wiki ya kwanza dhibiti wadudu waharibifu”

Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Mtwara Nanjiva Nzunda amesema kuwa sekta ya kilimo imekuwa ambapo mazao yaliyokuwa hayafanyi vizuri sasa yanalimwa mkoani hapa.


Mkoa Pia umedhamiria kuongeza uzalishaji wenye tija kwa Mazao ya kipaumbele kama Ufuta, Mbaazi, karanga, Alizeti, Choroko, korosho ,Soya na Mazao yote jamii ya kunde na kuimarisha huduma za  kilimo kwa  kuwawezesha maafisa ugani kwa kutumia tozo ya Sh.2 ya kila kilo ya korosho inayoenda halmashauri  ili kuwafikia wakulima na kuhakisisha kuwa kalenda ya mazao inafuatwa ambapo tutaandaa mafunzo ya  maafisa ugani 330.


Ambao Wilaya  hiyo imetoa hekari 100 kwa vijana 100 hii itasaidia kupandisha uzalishaji wa mazao mbalimbali katika mkoa wa Mtwara.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI