NA HADIJA OMARY, LINDI.
Kampuni ya kuchakata na kusafirisha Gesi asilia (Songas) imekabidhi vifaa vya michezo kwa kata ya Songosongo halmashauri ya Kilwa Mkoani Lindi vyenye thamani ya shilingi milioni 13 pamoja na fedha taslimu shilingi milioni 21 Kwa ajili ya uendeshaji wa ligi na tamasha la Michezo litalofanyika Desemba 1 siku ya UKIMWI duniani .
Akikabidhi vifaa hivyo Meneja wa mradi ya kijamii wa kampuni hiyo Nicodemus Chipakapaka amesema kampuni hiyo ya songas imekuwa ikijiwekea utaratibu wa kuchangia maswala mbali mbali kwa jamii katika sekta ya michezo, afya na Elimu
Amesema wamekuwa wakifanya hivyo ikiwa ni sehemu ya kurejesha kwa jamii katika shughuli wanazozifanya pamoja na kutambua jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuimarisha sekta hizo
Diwani kata ya Songosongo Hassan swalehe Ameeleza kuwa vifaa hivyo vinakwenda kukuza na kuinua vipaji kwa vijana wa kata hiyo ya Songo Songo
Kaimu Mkuu wa kitengo cha utamaduni sanaa na michezo Wilaya ya Kilwa Veneranda Kimaro amesema Katika kuendelea kukuza vipaji vya michezo kwa vijana tayari halmashauri imeshatenga bajeti ya ambayo inatekelezwa kupitia shughuli mbalimbali za kusimamia ligi kuanzia kwenye ngazi ya kata
Baadhi ya Viongozi wa kata ya Songosongo waliishukuru kampuni ya SONGAS kwa msaada huo walioutoa ambapo wamesema kuwa msaada huo umeendelea kuimarisha ushirikiano baina ya wanajamii wanaozunguka eneo la mradi pamoja na kampuni hiyo ya Songas
0 Comments