Header Ads Widget

TOSHCARCO NA TPBRC WAINGIA MAKUBALIANO, BONDIA LEILA MACHO ATOA OMBI KWA RAIS DKT SAMIA

Na Fatma Ally, Matukio Daima App, Dar

Kampuni ya usafirishaji mizigo Toshcargo leo wameingia makubaliano na Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini Tanzania (TPBRC) ya miaka miwili kudhamini mchezo wa boxing sambamba na kutoa tunzo za ngumi 2023/24 zenye mvuto wa aina yake.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Masoko wa Toshcargo Amitin Abubakar amesema kuwa, wamedhamini mchezo huo ili kutoa hamasa kwa watu waliokata tamaa sambamba na kuibua vipaji kwa vijana.


Amesema kuwa, utoaji wa tunzo hizo utafanyika rasmi mwezi June 2024 baada ya kuanza mchakato wa watu kupiga kura kuanzia March 2024 kwa kuchagua vipengele vinavyoshindaniwa, hivo ni muda muafaka sasa wa watu kuanza kufatilia mitandao ya kijamii ya Tpbrc na Toshcargo.

Kwa upande wake, Katibu wa Kamisheni wa Ngumi za Kulipwa (TPBRC ) George Lukindo amesema kuwa tunzo hizo ni mara ya kwanza kutolewa kwa mchezo huo hivyo, amewapongeza kwa kudhamini mchezo huo kwa miaka miwili ambapo zitatoa hamasa kubwa sana kwa watu pamoja na vijana kuweza kuupenda mchezo huo.


Aidha, ametaja miongoni mwa vipengele vitakavyoshindwa katika tunzo hizo ni pamoja na Kocha bora wa mwaka, chombo bora cha habari kitachoripoti taarifa za mchezo huo, mwandishi bora wa habari, Bondia bora wa kike na kiume, muandaaji bora wa mashindano pamoja na Kocha bora wa mwaka.

Akizungumza katika hafla hiyo, Bondia Leila Macho amemuomba Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluh Hassan kuunga mkono mchezo huo kwani wanafanya mazoezi katika mazingira magumu sambamba na kupata kipato kidogo ambacho hakikidhi mahitaji ya familia.


"Naipongeza Toshcargo kwa kutuona mabondia kwani mchezo huu kwenye masuala ya tunzo na udhamini tumesahaulika, Namuomba Rais Dkt, Samia kama ambavyo anatoa hamasa kwenye mpira wa miguu basi na huku kwenye bozing afanye maana naona tumesahaulika "amesema Bondia Leila.

Naye, Dulla Mbabe amesema kuwa, Toshcargo imefanya jambo kubwa kuliko kama kwani ugawaji wa tunzo wamekua wakiushuhudia zikitolewa kwa wanamuziki, wasanii wa bongo move, pamoja na wachezaji wa mpira sambamba na kupewa heshima, hivyo tunzo hizo zitatoa hasama ya wao kufanya vizuri kitaifa na kimataifa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI