NA CHAUSIKU SAID,MATUKIO DAIMAAPP MWANZA.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia Joseph Hezron mwenye umri (54) Mkazi wa Bukara Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza Kwa kosa la kuchoma moto nyumba Kwa wivu wa mapenzi na yeye kujaribu kujiua.
Akithibitisha kutokea Kwa tukio hilo kamanda wa Jeshi la Polisi Wilbroad Mtafungwa amesema kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Novemba 9 mwaka huu huku akimtuhumu mpenzi wake Lucy James umri (51) kuwa ana mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine.
Mtafungwa ameeleza kuwa Hezron alichoma moto nyumba hiyo alivyokuwa wakiishi na mpenzi wake na kuunguza vitu mbalimbali vyenye thamani ya sh, 16,000,000.
"Jeshi la Polisi limefanya uchunguzi na kubaini kuwa mwanaume aliyekuwa chanzo Cha tukio hilo hakuwa mpenzi wa Lucy bali alikuwa kaka yake, lakini kutokana na tabia ya wivu wa kimapenzi ndipo aliamua kufanya tukio hilo kinyume na sheria kanuni na taratibu za Nchi yetu" Alisema Mtafungwa.
Aidha Kwa upande mwingine ameeleza kuwa jeshi la polisi Kwa kushirikiana na jeshi la zima moto na uokoaji pamoja na wananchi walifanikiwa kuzima moto huo kabla haujaleta madhara makubwa.
Mtafungwa ametoa wito Kwa wananchi kuacha vitendo vya kujichukilia sheria mkononi na kutafuta njia sahihi ya kutatua migogoro hususani ya kimahusiano.
0 Comments