Na Matukio Daima Media , Mbeya
WAKAZI wawili wa Songea mkoani Ruvuma wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Mbeya kwa kosa la kujifanya Maafisa wa Jeshi la polisi Tanzania na kumtishia mkazi wa Mbalizi aitwaye Meck Mpepo na kumpora fedha taslimu shilingi 700,000 pamoja na simu tatu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Kamanda wa polisi mkoani Mbeya , Benjamin Kuzaga amesema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa katika Mji mdogo wa Mbalizi maeneo ya Stendi ya Tunduma wakati jeshi la polisi likifanya misako mbali mbali katika maeneo hayo.
Kamanda Kuzaga amewataja watu hao kuwa, Juma Mapunda (47),Said Wanyika (27) ambao wote ni wakazi wa Songea mkoani Ruvuma ambao walijifanya kujifanya maafisa wa jeshi la polisi Tanzania .
Aidha Kuzaga amesema waatuhumiwa walikamatwa katika Mji mdogo wa Mbalizi maeneo ya Stendi ya Tunduma katika misako inayoendelea kwa wananchi ambapo maafisa hao waliojifanya maafisa wea polisi walimkamata Meck Mpepo na kujitambulisha wao kuwa ni askari polisi kasha kumnyanganya fedha taslimu 700,000 pamoja na simu tatu.
Hata hivyo Kamanda Kuzaga amesema watuhumiwa wamehojiwa na kukiri kufanya matukio kadhaa ya utapeli katika mikoa ya Mbeya , songwe na Ruvuma kwa kujitambulisha kuwa ni maafisa wa polisi.
Mkazi wa Iyunga Jijini Mbeya , Boni Sanga amesema kuwa watu kama hao wamekuwa wakijitokeza katika jamii hivyo alipongeza jeshi la polisi kwa jitihada hizo na kuwaomba wananchi wenye taarifa za watu kama hao kutoa taarifa kwa jeshi la polisi kwani wamekuwa wakirudisha nyuma maendeleo ya wananchi .
Mwisho.
0 Comments