Na Editha Karlo,Geita
WAZEE Nchini wameiomba serikali kutatua au kumaliza changamoto zinazowakabili ikiwemo sera na miongozo ya haki zao.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Baraza la
wazwe nchini,Lameck Sendo kwa niaba ya wazee wenzake wakati wa kongamano la kitaifa la
wazee lililofanyika Mkoani Geita.
Alisema kupuuzwa kwa sera na miongozo ndiyo chanzo cha tatizo la matunzo duni,upweke,umaskini,ulimzi hafifu kwa wazee katika maeneo mbalimbali.
“Utakuta hata baadhi ya vyombo rasmi vya utawala kama mabaraza ya madiwani kwenye halmashauri unakuta wanapuuza sera na miongozo ya haki za wazee ikiwemo muongozo unao husu wazee wawili kuwemo katika mabaraza ya maamuzi”alisema
Mgeni rasmi katika kongamano hilo Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigella amewataka wakurugenzi katika halmashauri zote za mkoa huo kutekeleza sera na miongozo inayowataka wazee wawe na uwakirishi kwenye vikao vya maamuzi.
Shigella alisema kuwa serikali itaendelea kuboresha na kusimamia sera na miongozo kuhusu haki za wazew ikiwemo vita dhidi ya uonevu na ukatili katika kundi hilo muhimu kwenye jamii.
Maadhimisho ya siku ya wazee Kitaifa yanafanyika kesho Mkoani Geita na mgeni rasmi akiwa Waziri wa maendeleo ya jamii,jinsia wanawake na makundi maalum Dk Dorothy Gwajima.
MWISHO
0 Comments