NA WILLIUM PAUL, MOSHI.
MBUNGE wa Jimbo la Moshi vijijini wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro, Prof. Patrick Ndakidemi amechangia milioni 4.5 kwa ajili ya ujenzi wa jiko Katika shule ya sekondari ya Sungu.
Akimwakilisha Mbunge huyo katika mahafali ya 19 ya kidato cha nne katika shule hiyo, Diwani wa kata ya Kibosho mashariki, Christopher Ndakidemi alisema kuwa, kutokana na changamoto ya uchakavu wa jiko Mbunge ameamua kutoa kiasi hicho cha fedha ili kuanza kwa ujenzi wa jiko.
Ndakidemi alisema kuwa, katika kuhakikisha matatizo yanayowakabili wananchi yanaendelewa kupatiwa ufumbuzi Mbunge kwa kushirikiana na Serikali wameendelea kufanya juhudi kubwa za kutatua.
Alisema kuwa, Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hasani imeweza kutoa fedha nyingi kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo katika jimbo hilo ikiwamo miradi ya Afya, Elimu, Barabara na Kilimo.
Aidha Diwani huyo alitumia nafasi hiyo kuwasihi wanafunzi kujikita katika masomo ili kutimiza ndoto zao za badae na kuepuka kuingia katika vitendo vihovu vitakavyopelekea kuharibu ndoto zao.
Kwa upande wake, Mkuu wa shule akizungumza kwa niaba ya uongozi wa shule, James Warburg, alimshukuru mgeni rasmi pamoja na wageni wengine waliohuhudhuria katika mahafali hayo.
Wageni mbali mbali walihudhuria hafla hiyo wakiwemo viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Kata, bodi ya shule, waalimu wa shule za jirani pamoja na Afisa Mtendaji Kata na viongozi wengine wa Serikali ya Kijiji cha Sungu.
Mwisho..
0 Comments