Header Ads Widget

ASASI ZA KIRAIA KUHAMASISHA MATUMIZI BORA YA TEKNOLOJIA

Francis Kiwanga; Mkurugenzi wa mtendaji wa Foundation for civil society



Na Pamela Mollel, Arusha 


Asasi za kiraia zimeaswa kuhakikisha kuwa zinaendelea kuhamasisha jamii matumizi bora ya teknolojia ili teknolojia hizo ziwe msaada kwa jamii


Hayo yameelezwa jijini Arusha leo na mkurugenzi mtendaji wa Foundation for civil society Bw. Francis Kiwanga Wakati akiongea kwenye ufunguzi  wa mkutano wa wiki ya asasi za kiraia 


Francis alisema kuwa asasi za kiraia zina mchango mkubwa sana hasa kwenye sekta ya teknolojia ambapo wana uwezo wa kuisaida jamii kujua na kutambua aina ya teknolojia ambayo itaweza kuwasaida kwenye maendeleo


"kuna teknokojia ambazo zinaweza kusaidia jamii hizo ambazo zinaweza kusaidia jamii sasa zinatakiwa zipewe kipaumbele ili ziweze kuleta tija kwenye jamii"aliongeza


katika hatua nyingine aliitaka jamii kuhakikisha kuwa wanaenda sambamba na mabadiliki ya teknolojia ikiwa ni pamoja na kutumia teknolijia ambazo zitaongeza ufanisi zaidi.


Abubakar Ally; Mwakilishi wa kampuni ya Apple


Naye mwakilishi wa kampuni ya Apple ambaye pia naye aliongea katika mkutano, Bw. Abubakary Ally alisema kuwa jamii ya kitanzania inapaswa kuhakikisha inakubaliana na mabadiliko ya teknolojia ikiwa ni pamoja na kusimama na teknolojia moja ambayo itazaaa matunda


Abubakary alisema kuwa teknolojia ina nafasi kubwa katika kuleta maendeleo endapo tu mtumiaji atahakikisha kuwa anatumia vyema ikiwa ni pamoja na kupata ujuzi wa teknolijia  hiyo ipasavyo.


Awali akiongea kwa niaba ya Meya wa jiji la Arusha, diwani wa kata ya  ngarenaro Isaya Doita alisema kuwa kwa sasa teknolojia imekuwa kwa kiwango kikubwa sana lakini bado jamii inatakiwa kuhakikisha kuwa wanatumia teknolojia ipasavyo na sio kwenda kinyume na teknolojia  hizo. 


Doita alisema kuwa ili teknolojia ziweze kutumika ipasavyo hata kwa jamii ni muhimu kwa waaandishi wa habari lakini pia vyombo vya habari kuhakikisha kuwa vinaeleza umuhimu wa teknolojia  na matumizi yake ambayo ni mazuri ili teknolojia hizo ziweze kuleta mabadiliko ndani ya jamii. 

Isaya Doita; Diwani wa kata ya Ngarenaro jijini Arusha akiongea kwa niaba ya meya wa jiji




Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI