Na Scolastica Msewa, Kibaha.
Madereva wa wasio na uzoefu wa magari ya familia katika safari ndefu ni sababu ya ajali za Barabarani na kusababisha vifo au majeruhi nchini.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake Kibaha mkoani Pwani Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani ACP Pius Lutumo amesema ajali nyingi za safari ndefu za magari ya familia husababishwa na madereva wasio na uzoefu wa kuendesha magari katika safari ndefu.
Amesema hayo wakati akitoa taarifa ya ajali iliyosababisha Watu wa tatu wamepoteza maisha jana katika ajali ya barabarani ikihusisha magari mawili kugongana uso kwa uso huko Kijiji cha Mbala, Kata ya Vigwaza Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani majira ya saa 3 usiku.
Amesema ajali hiyo imehusisha gari dogo aina ya Kluger lenye namba T.478 DCQ ikitokea Iringa kwenda Dsm likiwa na watu 7 wa familia moja aligongana na gari lenye namba T.851 AQC aina ya Scania.
Katika ajali hiyo watu wanne walijeruhiwa ambao ni Amina Kondo miaka 77 na mtoto wa mwaka mmoja Abdallah Ally.
Mwisho..
0 Comments