![]() |
Askofu Dkt. Fredrick Shoo |
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT na Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini Askofu Fredrick Shoo amesema kuwa ni wajibu wa Kanisa kuwafundisha watoto neno la Mungu kama ilivyoelekezwa katika maandiko ya vitabu vitakatifu.
Askofu Shoo amesema hayo mwishoni mwa wiki wakati alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa Jimbo la Kilimanjaro kati Dayosisi ya Kaskazini Mkoani Kilimanjaro.
Aidha amesema kuwa watoto wanapaswa kulelewa katika njia mbadala hivyo ni wajibu wa kufanya hivyo kama ilivyoelekezwa katika maandiko.
"Na kwa hili pia nipende kuwapongeza na kuwatia moyo kwamba wengi mmejitoa na kujitolea ili muwajengee watoto Hawa msingi ambao hakuna atakeyeweza kuwaomdolea "Alisema Shoo.
Ameendelea kusema kuwa amewataka viongozi mbalimbali wa sharikani kuona umuhimu wa kuwafundisha watoto wa kipaimara Muhimu wa utunzaji wa mazingira na uumbaji wa Mungu kwa kupanda miti pale wanapoanza darasa la kipaimara.
"Lakini hata katika hili ninaona jinsi ambavyo pamoja na kuwafundisha mnatekeleza ule mpango wa Dayosisi wa kuotesha miti kwa ajili ya utunzaji wa mazingira hisusani katika kipindi hicho Cha mabadiliko ya Tabia ya nchi".Alisema.
Niendelee kusisitiza kwa sharika zote sio kwa watoto wa kipaimara tu Bali kwa vijana wote ili kulinda uoto wa asili na kutunza vyanzo vya maji
Mkuu wa Jimbo la kilimanjaro kati mchungaji Javason Mrema Amesema kuwa watoto wamekuwa hawahudhurii ibada zao kwa wingi ukilinhanisha na siku ya sikuu ya mikaeli na watoto ambapo amewataka viongozi kuhakikisha kuwa wanatumia mbinu mbadala ya kuwavuta watoto katika ibada kama kufanya matamasha ya watoto.
"Katika sikuu ya mikaeli na watoto idadi inaonekana kuongezeka zaidi inawezekana hata zaidi ya mara tatu ya idadi ya watoto katika siku za ibada za kawaida hii ni kuonyesha kwamba tukiweza kutumia fursa hii tunaweza kuwavuta watoto wengi kanisani"Alisema much.javason.
Ameendelea kusema kuwa Kuna njia ambazo zikifanywa zinaweza kuwavuta watoto kuhudhuria ibada bila kusubiri siku ya mikaeli na watotona ambapo amesema njia hizo ni pamoja na matamasha ya watoto ,mpango wa unjilisti wa nyumba kwa nyumba kwa watoto
Ameendelea kusema kuwa Mkuu wa wilaya ya Moshi Kisare Makori amesema kuwa Serikali inatambua mchango wa Kanisa katika kusukuma gurudumu la maendeleo na kusema kuwa ipo tayari kushirikiana na Kanisa pale wanapokwama .
0 Comments