Na Mwandishi, wetu.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa, Fakii Raphael Lulandala (MNEC), amezungumza na Viongozi wa Chama cha Mpira wa Wavu Tanzania (Tanzania Volleyball Association - TAVA) lengo likiwa ni kusikiliza changamoto zinazowakabili ili zipatiwe ufumbuzi.
Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo za Makao Makuu ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Upanga Jijini Dar es Salaam ambapo viongozi waliohudhuria ni Mwenyekiti Mhandisi, Magoti Mtani na pamoja na Laurance Safari, Katibu Mkuu.
Alisema kuwa, lengo lengo la mazungumzo hayo ni kusikiliza changamoto zao na kuzitafutia ufumbuzi ili kutafuta namna bora ya kuufanya mchezo wa wavu kuwa fursa ya ajira kwa vijana kama ilivyo kwa mpira wa miguu na zaidi kudumisha Ushirikiano kati ya Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi na (TAVA) ambao ni chanzo cha kukuza Vipaji vya Vijana wengi nchini.
Pamoja naye Katibu Mkuu alikuwa na Manaibu makatibu wakuu wa Jumuiya Mussa Mwakitinya (MNEC) Naibu Katibu Mkuu Bara na Mussa Haji Mussa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar.
Mwisho..
0 Comments