WANANCHI wa kata ya Mabogini jimbo la Moshi vijijini wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro wamempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hasani pamoja na Mbunge wa jimbo hilo, Prof. Patrick Ndakidemi kwa kuona umuhimu wa kujenga hospitali ya wilaya katika kata hiyo.
Wananchi hao ambao walidai kuwa walikuwa wakilazimika kutembea umbali mrefu hadi jimbo la Moshi mjini kupata huduma za afya katika hospitali ya rufaa ya mkoa Mawenzi hivyo kukamilika kwa ujenzi huo utawasaidia kupata huduma karibu zaidi.
"Tangu nchi hii ipate Uhuru hatujawahi kupata kituo cha afya wala hospitali lakini serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hasani kwa kushirikiana na Mbunge wetu Prof. Patrick Ndakidemi wameamua kuandika historia katika kata yetu ambapo katu haitoweza kufutika" alisema Amina Juma.
Naye Rashid Hasani alisema kuwa, kitendo kilichofanywa na serikali kujenga hospitali hiyo hawatakisahau na kuahidi kuwalipa viongozi hao kwa kutoa kura za kishindo kwa wagombea watakaotokana na chama cha Mapinduzi kuanzia uchaguzi wa serikali za mitaa mwakani na ule uchaguzi mkuu 2025.
Aidha wananchi hao walitumia pia nafasi hiyo kuikumbusha serikali kuhusu barabara ya Getifonga-Mabogoni-Kahe ambayo ipo kwenye ilani ya uchaguzi na inapaswa kujengwa kwa kiwango cha lami.
Mwisho..
0 Comments