![]() |
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Pwani imepokea malalamiko 126 katika kipindi cha miezi mitatu Julai hadi Septemba mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mjini Kibaha Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Pwani Sadiki Alli wakati akitoa taarifa ya miezi mitatu ya utendaji kazi kuanzia Julai hadi Septemba mwaka huu.
Alli amesema kati ya malalamiko hayo 92 yalihusu masuala ya rushwa huku 34 hayakuhusu rushwa na 27 wahusika walipewa ushauri manne yalifungwa na matatu yalihamishiwa idara nyingine.
Ametaja idara ambazo zinaongoza kwa kulalamikiwa kuwa ni Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) yenye malalamiko 44, na elimu 17, ardhi 15, ushirika sita, binafsi tano na polisi nne.
Idara nyingine ni afya na kilimo tatu, bandari, fedha, madini, maji, misitu na utawala malalamiko mawili kila moja, idara ya biashara, ofisi ya mkuu wa wilaya, mifugo, maendeleo ya jamii, Mamlaka ya Mapato TRA, uchukuzi, ujenzi, Tanesco, utalii na viwanda lalamiko moja moja kila idara.
0 Comments