Header Ads Widget

WATU 6 KATI YA 14 WALIOINGIA NCHINI KINYEMELA WAFARIKI KWA AJALI IYAYI NJOMBE

 


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Watu 6 ambao ni rai wa kigeni walioingia nchini kinyemela wamefariki kwa ajali  baada ya gari la mizigo kupinduka na wengine 8 kujeruhiwa katika kijiji cha Iyayi wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe.


Gari hilo lenye namba za usajili T. 501 AGJ aina ya Scania lililokuwa likielekea nchini Zambia lilipinduka na bado kiini cha ajali hiyo iliyotokea alfajiri ya kuamkia septemba 14 hakijajulikana ambapo dereva na kondakta wemetokomea kusiko julikana baada ya kukutwa na mkasa huo.



Mrakibu mwandamizi wa Uhamiaji mkoa wa Njombe Ibrahim Luwinzo Pamoja na Kamanda wa polisi mkoa  John Makuri Imori baada ya kufika eneo la tukio kufanya uokozi wanasema majira ya saa kumi na nusu alfajiri gari hilo lililobeba mizigo na raia wa kigeni imepata ajali na kusababisha janga hilo.



Mbali na kuaendelea kuwasaka wahusika wa biashara hiyo haramu kamanda wa uhamiaji anawataka raia wa Ethiopia kuacha kuingia kinyemela nchini kwasababu Tanzania imetoa ruhusa kwa watu hao kuingia wakiwa na nyaraka



Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe cloudia Kita anatoa onyo kwa watu wote wanaojihusisha na biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu. 


Wakazi wa kijiji cha Iyai akiwemo na Jacob Kilinyi ambaye ni mwenyekiti wa kijiji hicho   wanasema punde baada ya kupokea taarifa ya ajali hiyo wakafika eneo la tukio kwa ajili ya uokozi na kisha kuomba vyombo vya ulinzi na usalama kuongeza ukaguzi wa magari ya mizigo barabarani.



Mbali  na tukio hili Mwanzoni mwa mwaka huu zaidi ya wahamiaji haramu 60 walipata ajali katika kijiji cha Wangingombe  iliyokatisha maisha ya dereva wa gari dogo iliyogongana  na lori.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI