Header Ads Widget

VIONGOZI WA BARAZA LA WAMAASAI TANZANIA WAPINGA TAMASHA LA MAASAI FESTIVAL




 Na,Jusline Marco:Kilimanjaro



Baraza la Wamaasai Tanzania limelaani vikali TAMASHA LA MAASAI FESTIVAL  lililofanyika hivi karibuni jijini Arusha kwa makidai kwamba limefanyika kinyume na taratibu na sheria ya wamaasai kutokana na wahusika wa tamasha hilo kutokuwa wamaasai halisi.



Hayo yamejiri baada ya mkutano Mkuu wa Baraza hilo uliohusisha wazee, viongozi wa kimila (Malaigwanani) pamoja na akina mama wawakilishi katika Baraza hilo, ulioketi kupinga ukiukwaji huo wa tamaduni za wamaasai, ukiwa umelenga pia kuyokomeza mila potofu zinazoharibu taswira halisi ya kabila hilo na kurejesha nidhamu kwa vijana wa kimasai.



Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika katika mti wa kimila wa Orkolili,kijiji cha Olmelili Wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro na kukutanisha viongozi wa kabila la wamaasai walio kwenye Wilaya zote Tanzania,Mwenyekiti wa kitaifa wa jamii ya wamaasai Tanzania Joseph Labasilian Laizer ambaye pia ni Laigwanami Mkuu wa Malaigwanani Tanzania wa jamii ya Wamaasai amesema lengo la mkutano huo pamoja na kuwakjmbusha vijana wa kabila hilo kudumisha nidhamu na mila zao,wanajiandaa pia kuwa kufanya tamasha la kitamaduni la wamaasai wote wa Tanzania.



Aliongeza kuwa jamii ya wamasai ipo katika makundi 9 Tanzania ambapo katika makundi hayo 9 makundi 8 kati ya hayo makao yao makuu ni katika ofisi ya kimila iliyopo kwenye eneo la Oldonyorumuruwaki na hufanyika ibada za kimila kwa kila rika,na kundi la Ilarosa lina makao makuu eneo la Mianzini jijini Arusha.



Laizer alieleza kuwa kundi hilo la Ilarosa ni wenzao na wao hufanya mambo katika mambo yao ya kimila ikiwemo Kongamano lililofanyika hivi karibuni la Wamaasai ambalo wao hawajashiriki kutokana na kundi hilo kuwa siyo wamaasai halisi bali ni waarusha ambao kwa namna moja au nyingine wanaupotosha umma wa waganzania na kuwaaminisha kuwa wao ndio wamaasai wakati katika uhalisia siyo wamaasai.



"Nakanusha kuwa hao waliofanya tamasha hilo siyo wamaasai wenzetu hao ni waarusha na tamasha letu tutalifanya na watanzania wote wataliona na tutalifanyia katika maeneo yetu ya ibada ya mila na tunaiomba serikali ituunge mkono katika kufanikisha tamasha hilo ili watanzania waweze kutuona wamadai halisi tukiwa kwenye utamaduni wetu."alisema Laigwanani Mkuu Tanzania Joseph Labasilian Laizer



Akizungumzia suala la malisho kwa jamii hiyo ya Kifugaji, Laizer alisema kuwa wanakabiliwa na changamoto nyingi sana kulingana na mabadiliko ya tabianchi katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita ambapo pamoja na hayo maeneo ambayo serikali imeyataifisha na kufanya kuwa maeneo ya hifadhi ya wanyama inawapa wafugaji changamoto kubwa ikiwemo ya mifugo yao kukamatwa kwenye maeneo hayo,mifugo kufa kwa njaa kwa kukosa malisho,mifugo kikamatwa na kuyozwa faini ya hadi laki tano kwa kichwa kimoja cha ng'ombe jambo ambalo huwaumiza wafugaji.



Ameiomba serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt.Samia Suluhu Hassan kuiangalia jamii ya wamaasai kwa jicho la huruma kwasababu mifugo yao ikiteketea wao hawatakuwa na namna nyingine ya kuendesha maisha yao.



Kwa upande wake Katibu wa Viongozi wa Jamii ya Wamaasai Kitaifa Tanzania Jeremia Sendui Laizer alisema kuwa agenda ya mkutano huo ni kuweka mipango na misingi imara kwenye jamii na utamaduni na desturi katika nchi ya Tanzania sambamba na kuzungumzia changamoto na utatuzi katika maeneo mbalimbali nchi.



"Katika Mkutano wetu pia tumezungumzia nyanda za malisho za mifugo yetu na maisha na utamaduni wetu sisi wamasai kwa ujumla kuzunguka maeneo yote ya jamii ya wamaasai."alisema Ndugu Jeremia Sendui Laizer ambaye ni Katibu wa Viongozi wa Jamii ya wamaasai Kitaifa.



Nao baadhi ya vijana wa kimaasi ambao walihudhuria mkutano huo akiwemo Bahati Baraka kutoka Mkoani Mbeya Wilaya ya Mbarali wameeleza kuwa utumiaji wa tamaduni za kwao kwa watu ambao siyo wamaasai ni sawa na uharamia kwasababu jambo linapofanyika bila mwenyekiti wa kitaifa wa kabila husika kujua ni uharamia na ni jambo ambalo wao kama wamaasai hawapendezwi nalo hususani katika tamasha la Maasai festival lililofanyika jijini Arusha ambapo amesema hata uvaaji wa kisu kiunoni ni tofauti na wamaasai halisi wanavyovaa.



"Sisi wamasai tunavaa kisu upande wa kulia lakini ukiangalia katika tamasha lile wao wamevaa kisu upande wa kushoto na wanajiita ni wamaasai hiyo siyo  sawa na haipendezi mtu kutumia tamaduni za jamii nyingine tena kimakosa na kusema niwao kwa ajili tu ya kujipatia kipato huu ni uharamania na jamii yetu ya kimasai ina uongozi wake kutoka ngazi ya kitaifa ,Mkoa mpaka Wilaya ."Alisisitiza Baraka kijana wa Kimaasai rika la Morani



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI