Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Wafanyabiashara wa mazao ya misitu mkoani Njombe wamelalamikia kucheleweshwa kusafirisha mazao yao kutokana na Changamoto ya mtandao wakati wa kukata vibali vya kusafirisha mbao zao(TP).
Aidha changamoto za mlundikano wa vituo vya ukaguzi na umbali wa ofisi za kupata vibali hivyo Ni miongoni mwa vikwazo vilivyotajwa na Wafanyabiashara hao.
Wakizungumza mapema asubuhi baadhi ya wafanyabishara hao akiwemo Sophia Raymond,Erick Mtanga na Subira Kyando wamesema changamoto ya mtandao imewakwamisha kwa takribani wiki nzima na kuwasababishia hasara kwa kushindwa kusafirisha mzigo.
Audatus Kashamakula ni meneja wakala wa misitu Wilaya ya Njombe TFS ambaye amekiri kutokea kwa changamoto hiyo kwa muda wa siku mbili kwa nchi nzima lakini tayari imeshatatuliwa na kazi zinaendelea.
Kwa Upande wake mkuu wa mkoa wa Njombe Mhe.Antony Mtaka Baada ya kuwasikiliza wafanyabiashara hao ameagiza kushughulikiwa kwa changamoto hizo ikiwemo kuona njia mbadala ya kuwafanya wafanyabiashara hao kusafirisha mbao na nguzo zao pindi mtandao unapoleta shida ili kutokwamisha biashara nchini.
Hata hivyo Mtaka amesema mkoa wa Njombe unaotegemea mazao ya misitu kwa takribani asilimia 70 katika uchumi wake haupaswi kukwamishwa kwa namna yoyote hivyo wizara ya maliasili na Wizara ya Fedha zinapaswa kukutana kuona namna nzuri ya kushughulikia vikwazo hivyo.
0 Comments