NA MWANDISHI WETU, ZANZIBAR
CHAMA Cha ACT Wazalendo Kimeiomba Serikali ya Mapinduzi ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kusitisha bei mpya za utoaji wa Mizigo na Uingizwaji wa Gari katika bandari ya Malindi zilizotangazwa hivi karibuni na Kampuni ya Afrikan Global Logistics.
Hatua hiyo imefuatia malalamiko mbalimbali yaliyotolewa na Watumiaji wa Bandari ya Malindi juu ya kupandishiwa bei kwa Upakiaji na utoaji wa Mizigo kwa bandari ya Majahazi mara baada ya Serikali kukabidhi Shughuli zote za Uendeshaji wa Bandari hiyo kwa Mwekezaji Afrikan Global Logistics.
Akizungumza leo na Waandishi wa Habari Katibu wa Habari, Uenezi, Mawasiliano na Umma chama Cha Act Wazalendo Salimu Bimani chama chao kimepokea kwa uzito malalamiko ya Watumiaji wa Bandari na kuiomba Serikali kusitisha Mara moja bei hizo.
"Hofu imeibuka kwa Watumiaji wa Bandari baada ya bei mpya Sisi kama chama cha ACT Wazalendo tuinaiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kusitisha bei mpya za Utoaji na upakiaji wa Mizigo na uingizwaji wa gari bandarini kwa lengo la kushisha gharama za maisha kwa Wananchi wake," Amesema.
Pia wameiomba Serikali kuitisha kikao na wadau wote wa masuala ya Usafirishaji na uingizaji wa Mizigo bandarini ili kutafuta ufumbuzi wa masuala mbalimbali ya Bandari.
"Kikao baina ya Wafanyabiashara na kampuni ya AFrikan Global Logistics itapelekea kupata ufumbuzi wa tatizo hili na kurudisha Viwango vya gharama zilizokuwa zikilipwa hapo kabla ya tarehe 18 Septemba 2023, Amesema.
"Ikiwa hatua hizo zitashindikana, tunaitaka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuvunja mkataba na kampuni ya Afrikan Global Logistics na kurudisha uendeshaji wa bandari ya Malindi kwa shirika la bandari Zanzibar," Ameongeza.
Ameeleza kwa, Chama cha Act Wazalendo kinaamini kwamba Bandari ni Uchumi na kwa kiasi kikubwa inawanufasha Wazanzibari na Uchumi wa Zanzibar.
" Wanzanzibar hususani Wafanyabiashara wanategemea bandari ya Malindi ya Zanzibar kwa kupakia na kupakua bidhaa zao, hivyo basi hatutakubali kuona uchumi wa Zanzibar unauliwa kwa manufaa ya watu wachache," Ameeleza.
0 Comments