Header Ads Widget

VITUO VYA POLISI KUWEKWA CCTV CAMERA KUWABAINI ASKARI AMBAO SI WAADILIFU


Matukio Daima App, Dar es Salaam.

WAHITIMU wa Mafunzo wa Sajenti Jeshi la Polisi Tanzania, wametakiwa kuwa waadilifu na kujiepusha na Vitendo vya Rushwa  ambavyo vimekithiri kwa Baadhi ya Askari wa Polisi.


Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Kaspar Mmuya,  katika hafla ya kuwatunuku vyeo askari wa jeshi la Polisi waliomaliza mafunzo ya uongozi mdogo wa Sajenti 774 katika viwanja vya Polisi Ziwani.

Amesema wapo askari wa jeshi hilo wanafanya kazi vizuri lakini wapo wachache ambao wanachafua sifa yao na chombo hicho kwa kuomba rushwa.  


Alibainisha kuwa rushwa wataendelea kuidhibiti kwa kuweka mifumo ya kielektroniki ikiwemo CCTV Camera popote watakapofanya kazi ikiwemo vituo vya polisi.  


“Tutaweka kamera nje ndani na tutaweka mifumo ya kuanza kumsikiliza mteja taarifa zake ambazo zitasomeka na mlolongo wote wa haki jinai tutaona uharakishaji wa upelelezi wa kesi zote hakikisheni mnafanya majukumu yenu kwa ueledi na wakati na ukikaa na faili utajulikana wewe ndio uliyesababisha,” alisema.


Alisema askari hatoweza kufanya uonevu wowote kwa mifumo ambayo itaweka itaweza kuonesha mambo yake yote wakati anauhudumia raia.


 Aidha amebeinisha kwamba,  asingependa kuwaona askari hao wanafikiria mshahara na cheti bali ni kufikiria maarifa yanamjengea ujuzi na kumfanya kuwa mahiri katika utendaji kazi wa kazi zake.


Katika hafla hiyo Katibu Kaspar aliwatunuku vyeti wanafunzi saba waliofanya vizuri zaidi ambao ni Visent Daniel, Matha Zakaria, Nicolas Charles Silimba, Tatu Omar Mwalim, Anjelina Samuel Mkumbo, Rushita Lugiko Yussuf na Joseph Jastin Jordan.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS