Header Ads Widget

MWENYEKITI UVCCM AZINDUA 'DOOR TO DOOR'..

 Na Gift Mongi MATUKIODAIMA APP MOSHI.

Umoja wa vijana wa chama cha Mapinduzi (UVCCM)wilaya ya Moshi Vijijini umezindua aina mpya ya kampeni zilizopewa jina la 'door to door' katika kampeni za uchaguzi mdogo katika kata ya Old Moshi Magharibi.

Aina hii inaelezwa kuwa lengo lake kubwa ni kuhakikisha kila mkazi kwenye kata hiyo anafikiwa na kuombwa kura ya ndio kupelekewa uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.


Uzinduzi wa aina hiyo ya kampeni umefanywa na mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama hicho wilaya ya Moshi Vijijini Yuvenail Shirima na kuwa sio lazima kuomba kura katika mikutano pekee bali ni pamoja na kuwafuata wapiga kura sehemu walipo.

'Hatufanyi siasa kimazoea zipo njia nyingi za kuomba kura ikiwemo hii tuliyozindua 'door to door' na hapa tutawafikia wapiga kura wengi zaidi kuliko kusubiria mikutano ya hadhara.

Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo lengo ni kuhakikisha kuwa chama hicho kinaibuka mshindi katika uchaguzi na kuwa ushindi ni lazima uwe wa kishindo.

'Staili hii mpya inaenda kuleta matokeo mazuri na lazima tuikomboe hii kata yetu na ushindi ni dhahiri utakuwa mnono maadamu wapiga kura wanatuelewa'alisema

 Janeth Mushi ambaye ni mkazi wa eneo hilo alisema Wana imani na chama cha mapinduzi (CCM)na kuwa kitaenda kuibuka kidedea katika uchaguzi huo mdogo.

'Hakuna sababu kwa nini CCM isishinde kwani tayari tumeona miradi mbali mbali ya kimaendeleo ikitekelezwa katika kata yetu hii ni lazima tukaendelea tulipokuwa tumeishia'alisema 

Menyasumba Macha alikuwa diwani wa tatu wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro kupoteza maisha na kufanya idadi ya kata zilizoko wazi kufikia tatu, kata hizo ni pamoja na Old Moshi Magharibi (Moshi), Kalimawe na Njoro (Same).

Tayari chama cha mapinduzi (CCM)kimeshazindua kampeni zake katika kata husika na kuwa wamejipanga kuhakikisha kata zote hizo zinarudi katika mikono yake kwani hapo awali' zote zilikuwa chini ya chama hicho

MWISHO.







Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI