Header Ads Widget

VIJANA WATAKIWA KULINDA AMANI YA NCHI

 


NA MWANDISHI WETU,ZANZIBAR


VIJANA  Nchini washauriwa kufahamu kuwa, Viongozi na waasisi wa Taifa walifanya kazi kubwa ya Kuhakikisha Mapinduzi na Uhuru unapatikana hivyo wajibu wao kuhakikisha wanatunza na kulinda amani ya nchi.


Aidha Vijana wameshauriwa kutokubali kutumika na baadhi ya watu katika kuharibu Amani, Umoja na Mshakamano uliopo hivi sasa  Nchini.


Wito huo umetolewa leo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi,Uchumi na Uwekezaji Zanzibar Mudrik Ramadhani Soraga katika Kongamano la kuadhimisha Siku ya Amani Kimataifa ambapo kitaifa Siku hiyo imeadhimishwa Zanzibar  katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul -Wakil Kikwajuni.


Waziri Soraga amesema kuwa, Serikali inatambua mchango wa Vijana katika kulinda Amani pamoja na ustawi wa uchumi wa Nchi.


"Taifa lolote linajivunia kuwepo kwa Vijana na sisi Tanzania tunatambua mchango wa Vijana katika kulinda Amani pamoja na ujenzi wa Uchumi wa Nchi," amesema.


Ameeleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatekeleza Mipango mbalimbali ya kuwainua kiuchumi na kuondokana na utegemezi.


"Vijana wanapokosa Ajira husabisha kuvuruga kwa Amani ya Nchi hivyo Serikali ya Mainduzi ya Zanzibar inatekeleza mipango ya kuwawezesha kielimu na Mitaji vijana ili kujiuinua kimaisha,"ameeleza.


Maadhimisho ya Siku ya Amani kwa mwaka huu yameshirikia makundi mbalimbali ya Vijana,Asasi za Kiraia pamoja na Wanafunzi kutoka Shule mbalimbali za Msingi na Sekondari.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI