Header Ads Widget

MAAFISA NA ASKARI 13 WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MKOANI MTWARA WAMEVISHWA VYEO.

Mtwara.Maafisa na askari 13 wa jeshi la zimamoto na ukoaji mkoani Mtwara wamevalishwa vyeo na Mrakibu msaudizi wa jeshi la zimamoto na Uokoaji Oissa Singili ambaye ni Kaimu kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkani humo katika siku ya kumbukizi ya wazimamoto walio fariki wakiwa katika majukumu yao.

Katika maazimisho hayo yanayo fanyika duniani kote tarehe   04.05  ya kila mwaka leo  Mayi 04 yameaazimishwa mkoani Mtwara kwa kuwavisha vyeo maafisa  na askari 13 wajeshi la zimamoto na uokoaji mkoani humo sambamba na kufanya maandamano.

Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoti na  uokoaji  Oissa  Singili ambaye ni Kaimu  kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji  mkoa wa Mtwara amewavisha vyeo maafisa na askari 13 wa jeshi hilo mkoani humo kwaniaba ya afande kamishana jenerali wa jeshi la zimamoto na ukoaji John Masunga(CGF)

Katika tukio hilo  Mrakibu wa jeshi la zimamoto na uokoaji Oissa Singili amewaomba wananchi watoe tarifa za majanga mapema na sio waanze kupambana wenyewe kwanza.

"Nawaomba wananchi watoe taarifa mapema nasio waanze kupambana wenyewe kwanza kabla yakutoa taarifa ya majanga yanapotokea kwaajili ya maokozi iwe ni moto,maokozi mengine kwakupiga simu namba  114 askari wako tayari kutekeleza majukumu.Tunaomba jamii itambue majukumu ya  jeshi la zimamoto na uokoaji  wanapotekeleza majukumu yao"amesema Oissa kaimu kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji.

Kaimu kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani Mtwara amesema maazimisho ya siku hiyo ya kuwakumbuka wazimamoto walio poteza maisha wakati wakitekeleza majuiumu yao walianza  tokea April 28 kwakufanya shuguli mbalimbali ikiwemo kuwatembelea walio pata majanga  na kufanya usafi na  leo Meyi 04,2025 yamefikia tamati 

"Lengo lakuazimisha siku hii ya wazimamoto kuwaenzi wazimamoto  duniani kuna mwaka maafisa na askari wakiwa wanatekeleza majukumu yao walipoteza maisha kwahiyo siku hii nimuhimu katika kuwaenzi.Pia tumefanya usafi maeneo mbalimbali tumewatembelea walio pata majanga kwa lengo la kuwatia moyo.Jeshi la zimamoto halifanyi kazi peke yao linashirikiana na wadau mbalimbali kama msalaba mwekundu,jeshi la polisi."amesema Oissa

Oissa amesema katika maazimisho hayo amewavisha vyeo  maafisa na askari 13 kwa niamba ya Kamishina jenerali wa Jeshi la zimamoto na uokoaji John Massunga.

"Leo imekuwa ni siku ya   baraka kwa maafisa na askari 13 kwaniaba ya Kamisha jenerali nimewavisha vyeo  askari  6 walio toka cheo cha  mkaguzi na kwenda kuwa mrakibu masaidizi wa jeshi la zimamoto na uokoaji ,wawili wametoka cheo cha  stesheni sajenti  kwanda kuwa mkaguzi msaidizi na wengine 5 wametoka cheo cha sajenti na kuwa stesheni sajenti;lengo ni wapa moyo na kuwaongezea majukumu yao"amesema Oissa Kaimu kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani Mtwara.

Baadha ya maafisa na askari  walio vishwa vyeo wamesema wako tayari kwenda kuzitumikia nafasi zao na wameshukuru kwa kupandishwa vyeo.

Bilhah Chailla ambaye amepandishwa cheo kutoka kuwa mkaguzi na sasa Mrakibu masaidizi wa jeshi la zimamoto na uokoaji amesema majukuku yameongezeka na yuko tayari kutekeleza majukumu hayo.

"Nipo tayari ,nipo timamu  kwenda kutekeleza majukumu yangu  na   kutimiza majukumu na kuwajibika.Nitoe rahi kwa wanawake wenzangu majeshi sio yawanaume hata wanawake tunaweza mimi nimefika hapa kwa jitihada zangu mwenyewe zinapotokea nafasi wasisite kujitokeza kuomba"amesema  Chailla mrakibu msaidizi wa jeshi la zimamoto na uokoaji.

Kwa upandewake Yona Magazi afisa Uokoaji na zimamoto wilayani Masasi  ambaye amepandishwa cheo kutoka kuwa Mkaguzi hadi  Mrakibu msaidizi jeshi la zimamoto na uokoaji amesema kupandishwa cheo kwake ni deni lakini pia sio mwisho ataendelea kupambana ili apande cheo zaidi.

"Mtumishi yoyote anapopanda cheo ni lazima atakuwa na furaha hata mimi ninafuraha lakini hili ni deni natakiwa kuhakikisha natekeleza ambayo yanastahiki kuwa na cheo hiki.Nimjipanga kutekeleza majukumu yangu zaidi kwasababu cheo hiki sio mwisho nitaendelea kuchapa kazi kuhakikisha napanda kufika juu kabisa"amesema 


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI