Header Ads Widget

TANZANIA YAINGIZA MABILIONI KUPITIA VIUATILIFU VYA KUUA MAZALIA YA MBU.

 


TANZANIA imepata kiasi cha shilingi bilioni 3.3 kwa kuuza lita 272, 444 za viuatilifu vya vya kuua mazalia ya mbu kupitia kiwanda cha Tanzania Biotech Products Ltd (TPBL).


Hayo yalisemwa na Dk Ashatu Kijaji wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea mafanikio mipango na mikakati ya kiwanda hicho cha (TPBL) kinachojihusisha kuzalisha viwatilifu vya kuuwa mazalia ya mbu ambacho kiko chini ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) kilichopo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.


Alisema kuwa dawa hiyo imeuzwa kwenye nchi saba za Afrika za Kenya, Angola, Niger, Botswana, Namibia Msumbiji na Swatini huku mazungumzo na nchi ya Uganda ikiwa kwenye mazungumzo ya kununua dawa hiyo.


Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa NDC Dk Nicoluas Shombe alisema kuwa kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalishaji wa dawa hiyo ni milioni sita kwa mwaka na kilianza uzalishaji mwaka 2017 kilianzishwa kwa malengo ya kukabiliana na ugonjwa wa maleria kwa kuua mazalia ya mbu ili ifikapo 2025 maambukizi yawe 0 na cha kipekee Afrika na duniani vikiwa ni vitatu tu kikiwa kinazalisha dawa za kibaiolojia.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI