Header Ads Widget

MKUTANO MKUU WA AHMADIYYA KUANZA KESHO

 


Na fatma Ally, Matukio DaimaApp, Dar


Mkutano Mkuu wa 52 wa Jumuiya ya Kiislam Ahmadiyya unatarajiwa kuanza Sept 29 hadi Octoba 1,2023 Kitonga, Msongola, Manispaa ya Ilala ambapo washiriki zaidi 5000 kutoka nchi mbalimbali wanatarajiwa kuhudhuria ikiwemo, Ghana, Kenya na Uganda.


Akizungumza jijini Dar es Salaam, mbele ya waandishi wa habari Naibu Amir Abdulrahman Mohamed Ame amesema kuwa, Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Mpango anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wa jalsa hiyo ambapo mambo mbalimbali yatazungumzwa.


Amesema kuwa, kupitia mkutano huo waumini watapata nafasi ya kusikiliza hotuba na nasaha za wataalamu wa Jumuiya ambapo miongoni mwa mambo yatakayozungumzwa ni namna bora ya kuwalea watoto ikiwemo kujali elimu yao ya dini na sekula yaani kujitahidi kuwa raia wema kwa kuishi kwa amani na watu wote na kuwa watiifu kwa sheria za nchi.



Hata hivyo, amesema kupitia mkutano huo waumini watakumbushwa juu ya umuhimu wa kujiepusha kuchanganya dini na siasa kwani jambo hilo huleta mkanganyiko na kuzalisha mianya ya ama wanasiasa kuitumia dini vibaya au watu wa dini kuitumia siasa vibaya kwa ajili ya maslahi yao binafsi.


Aidha amesema kuwa kauli mbiyu ya Jalsa ya mwaka huu nchini Tanzania ni " Tawheed ya kweli haiwezi kusimamishwa na bila ya Ukhalifa" ikiwa na maana ya kuwa mfumo wa Ukhalifa ulioanzishwa na Mwenyezi Mungu tangu zama za Nabii Adam ndio njia pekee ambayo Mwenyezi Mungu hudhihirisha umoja wake duniani ambapo Tawheed ya kweli itasimamishwa kupitia ukhalifa ulioanzishwa tena na Mwenyezi Mungu katika uislam sawa na ahadi iliyotolewa na Mtume Muhammad (S.A.W).



Aidha amesema kuwa Jumuiya ya waislam wa Ahmadiyya ni Jumuiya ya Kimataifa inayopatikana kwenye zaidi ya nchi 212 duniani ikiwa nchini ya kiongozi mmoja( Khalifa Mtukufu) 


"Lengo lake kuu ni kutangaza kwa amani ujumbe sahihi wa Islam duniani kote na kuwa mstari wa mbele katika kupinga maana zisizo sahihi zinazonasibishwa na mafundisho ya uislam kama vile dhana potofu za ugaidi na misimamo mikali isiyovumilia wengine" amesema Naib Amir Ahmadiyya Muslim Jamaat Tanzania Abdulrahman 



Awali akisoma ujumbe wa Kiongozi Mkuu wa Ahmadiyya Duniani, Amir  Missionary Inharge wa Ahmadiyya Muislim Jamaat Tanzania Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry amesema kuwa, Mkusanyiko huo umejengwa juu ya uungwaji mkono kamili wa ukweli na uenezaji wa uislam ambapo jiwe la msingi la jumuuiya hiyo limewekwa na mwenyezi Mungu.


"Nimuhimu kwamba mnufaike kikamilifu na mwenendo ya Jalsa hii ili kujifunza jinsi ya kuboresha viwango vyenu vya kiroho na kimaadili , kuwa bora katika kufanya vitendo vya ucha Mungu ni hivyo kupata ukaribu kwa mwenyezi Mungu Mtukufu"imeeleza taarifa hiyo.


Aidha taarifa hiyo pia imeongeza washiriki wa Jalsa hiyo wanapaswa kuzingatia wajibu wao kuhusu mahubiri ambayo ni muhimu kwa kila ahmadiyya kupanga nakubuni njia mpya na zenye hekima kueneza ujumbe wa amani wa Islam ahmadiyya kote Tanzania na nchi jirani.





Naye, Amir Ahmadiyya Muslim Ghana Mohammed Bin Salih amesema kuwa amefurahishwa kupewa mualiko wa kuja kushiriki Jalsa nchini Tanzania huku akisema kuwa mkusanyiko huo unasaidia vijana kubadilika kimalezi na kiimani amewasisitiza Watanzania kujitokeza kushirikia mkusanyiko huo.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI