Header Ads Widget

MANDONGA APIGWA TENA ZANZIBAR.


Na Simon Joshua - Matukio Daima App, Zanzibar.

Bondia mwenye mbwembwe nchini Tanzania Karim Mandonga amepigwa kwa pointi na Othmani Kiluwa kwenye pambano maalum la Uzinduzi wa mchezo wa Ngumi Visiwani Zanzibar lililopigwa kwenye uwanja wa Mao Zedong.


Kwenye mchezo huo Majaji wote watatu wamempa ushindi Kiluwa kwa pointi 55-56, 56-58 na 55-59.


Hichi ni kipigo cha tatu mfululizo kwa mwaka huu Mandonga kupigwa ambapo alianzwa kupigwa Julai 22 alipoteza pambano la marudiano na Mkenya Daniel Wanyonyi, na Julai 29 alipoteza pambano dhidi ya mganda Moses Golola na Agost 27 kupigwa na Kiluwa.


Una mshauri nini Mandonga Mtu Kazi aendelee kupigana au apumzike kwanza?


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS