Na Gabriel Kilamlya Matukio Daima App, Njombe
Wakati serikali ikiendelea kuimarisha miundombinu katika sekta ya elimu nchini,taasisi za fedha zimetakiwa kuona uwezekano wa kuwasaidia walimu ambao wanajikuta wanaingia kwenye changamoto kubwa ya kukopa mikopo ya mitaani ambayo imekuwa ikiwakosesha amani na wengine kukimbia hadi makazi yao.
Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wakati wa semina kwa walimu chini ya Benki ya NMB kupitia programu maalumu ya Mwalimu spesho amesema ipo haja ya Benki hiyo kuwapa mikopo nafuu walimu pamoja na kuwaandaa wanasaikolojia kwa ajili ya kuwasadia walimu ambao wakati mwingine wanajikuta wanashindwa kufanyakazi vyema kutokana na mikopo Kausha damu.
Meneja wa NMB kanda ya nyanda za juu kusini Straton Chilongola amesema walimu wamekuwa wadau wakubwa na muhimu katika taasisi yao na hivyo wameona ulazima wa kuwapa kipaumbele katika huduma za fedha.
Ally Ngingite ni meneja mwandamizi huduma kwa wateja binafsi ambaye anasema benki hiyo imeweka mikopo maalumu kwa walimu ikiwemo ya vyombo vya usafiri ili kuwarahisishia suala la usafiri wawapo kazini.
Kwa upande wao baadhi ya walimu mkoani Njombe akiwemo Danford Chaula na Tumain Sanga wamesema mikopo kausha damu imewaingiza walimu wengi katika matatizo makubwa yanayoshusha molari ya kazi kutokana na kudharirishwa pindi wanapodaiwa madeni hivyo Wanaamini NMB iwe kimbilio lao.
Hata Hivyo Mwalimu Sanga amesema kuna wakati walimu wanajifichi chini ya madawati mbele ya wanafunzi pindi wadai madeni wa mikopo kausha damu wanapofika jambo ambalo linawaingiza kwenye msongo mkubwa wa mawazo.
Benki ya NMB imeanzisha programu maalumu ya Mshiko fasta kupitia simu ya kiganjani ambapo mteja anaweza kukopa wakati wowote kuanzia shilingi elfu moja hadi laki tano.
0 Comments