Teddy Kilanga ARUSHA
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza wawakilishi Zanzibar,Dk Hassan ali Mwinyi amewataka wananchi na viongozi mbalombali kutumia maadhimisho ya siku ya kupambana na rushwa barani Afrika kujitathmini juu ya hatua walizochukua katika kupambana na vitendo vya rushwa katika maeneo yao.
Akizungumza kwa niaba ya Rais Mwinyi, jijini Arusha katika uzinduzi wa maadhimisho hayo ya siku tatu yaliyoanza julai 9 hadi 11,2023,Makamu wa wapili wa Rais Zanzibar, Hemed Suleiman alisema ni vyema wanachi wakatumia maadhimisho hayo katika kujitathmini pamoja na kuweka mikakati ya kupunguza vitendo hivyo.
"Maadhimisho haya yameandaliwa kwa ajili yetu sisi wahusika kwani ni muda muhafaka wa kujipanga zaidi katika kupambana na rushwa hivy kila mwanachi kutoka nchi za Afrika na sio Taasisi za rushwa pekekee,"alisema Makamu wa pili wa Zanzibar.
Kwa upande wake Waziri wa nchi Ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora,George Smbachawene alisema Tanzania iko tayari kushirikiana na mataifa mengine katika mapambano dhidi ya rushwa.
Mkurugenzi mkuu wa Takukuru,CP.Salum Hamduni alisema Julai 11 kila mwaka ni siku iliyotengwa na Umoja wa Afrika kuadhimisha mapambano dhidi ya rushwa barani Afrika ambapo ni maadhimio ya mkutano wa 29 wa wakuu wa nchi za umoja wa Afrika uliofanyika Adis ababa nchini Ethiopia julai 3 hadi 4,2017.
"Kauli mbiu ya mwaka huu katika maadhimisho ni mafanikio baada ya miaka 20 wa utekelezaji wa mkataba wa Umoja wa Afrika wa kuzuia kupambana na rushwa na Matarajio yake,"alisema Mkurugenzi Hamduni.
Mkurugenzi Hamduni amesema kuwa maadhimisho ya mwaka 2023 yataambana na shughuli mbalimbali ikiwemo maonyesho ya asasi za kiraia ambapo yamewekwa mahususi katika kutoa elimu ya masuala ya rushwa kwa wananchi.
Mkurugenzi huyo amesema Julai 10 kutakuwa na kongamano la wadau litakalofunguliwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora,George Smbachawene ambapo litahusisha majadiliano ya mada mbalimbali ikiwemo uzoefu wa Taasisi za kupambana n rushwa barani Afrika kwa miaka 20 iliyopita tangu kusainiwa kwa mkataba wa umoja wa Afrika wa kupambana na rushwa.
Amesema mada nyingine ni pamoja na uzoefu katika urejeshwaji mali zilizopatokana kwa njia ya rushwa na mazalia yake,Mchango wa Asasi za kiraia katika kuendeleza mapambano dhidi ya rushwa,mchango wa vijana katika mapambano dhidi ya rushwa katika ulimwengu wa Kidigitali.
Pia amesema mada nyingine ni matumaini baada ya miaka 20 ya utekelezaji wa mkataba wa umoja wa Afrika katika mapambano dhidi ya rushwa,athari za rushwa katika sekta ya elimu kupata uzoefu katika nchi wananchama, Utafiti katika kijikita katika ushahidi kuhusiana na mikakati dhidi ya kupambana na rushwa pamoja na tathmini ya mchango wa Taasisi za kimataifa na wadau wa maendeleo katika utekelezaji wa mkataba wa Umoja wa Afrika katika kupambana na rushwa.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa kuzuia na uhujumu uchumi Zanzibar(ZAECA) Ali Abdalah Ali alisema mikakati yao ni kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ikiwemo katika Taasisi za umma na binafsi katika kudhibiti mianya ya rushwa.
Baadhi ya wakazi wa mkoa wa Arusha wamesema wanapata changamoto ya kukabiliana na vitendo vya rushwa kutokana na kuwa na uelewa mdogo wa masuala ya rushwa hali inayopelekea jamii kuamini rushwa ni haki yao.
0 Comments