Na,Jusline Marco;Arusha
Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt.Dorothy Gwajima ameitaka Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru kujikita katika kutoa elimu kwenye maeneo ya ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto pamoja na masuala ya uwezeshaji wanawake na jamii kiuchumi.
Dkt.Dorothy ametoa rai hiyo wakati akizindua sherehe za miaka 60 ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru, uzinduzi wa nembo iliyoboreshwa ambapo ameitaka pia kujikuta katika kuhamasisha maadili ya Taifa kwa kuzingatia Mila, Desturi na Tamaduni za nchi ikiwa ni pamoja na kufufua shughuli za Inten-ship kwa kuwawezesha maafisa maendeo ya jamii kuweza kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa.
"Sasa tuende tukaangalie tunakuwaje daraja la kutoka kwenye fursa zilizopo na kufika kwa wananchi na kuitangaza Tengeru inapokuwa katika miaka 60 tangu kuanzishwa kwake "Alisisitiza Dkt.Dorothy Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum
Dkt.Gwajima amesema uanzishwaji wa Wizara hiyo ni ili kuongeza msukumo na kasi ya utekekezaji wa shughuli za maendeleo ya jamii ambapo Rais Dkt. Samia ametoa kibali cha ajira kwa maafisa maendeleo ya jamii 800 kwa wakati mmoja ili kusadifu nia ya Dkt.Samia katika kuendelea kuimarisha sekta ya maendeleo ya jamii nchini.
Ameongeza kwa kukipongeza chuo cha maendeleo ya jamii Tengeru kwa kubuni wazo la kuwa na mfuko wa udhamini masomo wa maendeleo ambapo amesema ni matumaini yake mfuko huo utakuwa msaada mkubwa katika kusaidia wanafunzi wanaotoka katika mazingira magumu kuweza kufanikisha ndoto zao za kupata mafunzo katika vyuo vya kati na vya juu.
Katika hatua nyingine Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dkt.Dorothy Gwajima wakati akiwatunuku vyeti wahitimu 103 wa mafunzo ya huduma ndogo za kifedha CMGs yaliyotolewa na shirika la Center fo VICOBA and Enterprises Development kwa kushirikiana na chuo cha maendeleo ya jamii Tengeru ambapo amesema upatikanaji wa maendeleo ya jamii yanategemea mfumo madhubuti wa sekta ya fedha ambayo ndiyo kiungo muhimu katika sekta ya maendeleo ya jamii.
Dkt.Gwajima ameeleza kuwa sera ya maendeleo ya jamii ya mwaka 1996 inatanbua uhusiano kati ya sekta ya fedha na maendeleo ya jamii huku baadhi ya malengo yakiwa ni kuweesha wananchi kushiriki katika mifumo ya kiuchumi kwa kubadilisha bidhaa na huduma za fedha ili kuinua hali zao za maisha,kuwezesha kutumia vipato vyao kwa uangalifu na kuweka utaratibu wa kuweka akiba.
Ameongeza kuwa serikali kupitia wizara ya fedha imeweka mazingira mazuri kupitia sera,sheria,miongozi,mipango na program mbalimbali ili kuwezesha ustawi wa sekta ya fedha kwaajili ya maendeleo ya jamii ambapo amesema pamoja na uhusiano uliopo,kwa upande wa maendeleo ya jamii bado jitihada za kutosha hajizafanyika ili kuweza kubaini fursa zilizopo katika sekta ya fedha.
Amebainisha kuwa malengo ya mafunzo hayo ni kutoa elimu elimu ya fedha na kuwajengea uwezo washiriki juu ya uendeshaji na usimamizi wa vikundi vya kijamii vya huduma ndogo za fedha ambapo amesema elimu ya fedha ni muhimu sana kwa maendeleo ya jamii.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya jamii,jinsia,wanawake na makundi maalum Dkt.John Anthony Jingu amesema kuwa kada ha maendeleo ya jamii ni muhimu katika maendeleo ya nchi kwani kazi kubwa ha maafisa maendeleo ya jamii ikiwa ni kubadilisha fikra za watu na kujenga fikra chana na kuleta mabadiliko chanya katika jamii hivyo wanalo jukumu kubwa ka kuhakikisha changamoto zote kubwa katika jamii zinatatuliwa.
Dkt.Jingu ameongeza kuwa kwa kuahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa taasisi ya maendeleo ya jamii Tengeru na taasisi nyingine za maendeleo ya jamii pamoja na wadau wengine kuhakikisha malengo ya Rais Dkt.Samia Suluhu katika kuleta maendeleo ya jamii kwenye kukuza maendeleo ya nchi yaweze kutimia.
Naye Dkt.Bakari George Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru amesema kuwa taasisi hiyo kwa kutambua uhusiano uliopo kati ya sekta ya maendeleo ya jamii na sekta ya fedha kwa vipindi tofauti imekuwa ikichukuwa hatua mbalimbali ikiwa ni kuingia makubaliano na shirika la CeveDe ili kushirikiana kwa pamoja katika kuendesha mafunzo ya muda mfupi kuhusu huduma ndogo za fedha pamoja na afua mbalimbali zinazotokana na huduma ndogo za fedha mnamo mwaka 2022.
Aidha amesema katika kuanza utekelezaji wa makubaliano hayo taasisi ya maendeleo ya jamii Tengeru pamoja na shirika CeveDe kupitia kituo cha huduma tandano ubunifu wa kidigitali iliandaa mafunzo kwa wanafunzi kwa lengo la kutoa elimu ya fedha kwa washiriki na kuwajengea uwezo washiriki juu wa uendeshaji na usimamizi wa vikundi vya kijamii vya huduma ndogo ya fedha ambapo utoaji wa mafunzo hayo ni utekelezaji ea sheria,sera na miongozo katika sekta ya fedha.
Ameeleza kuwa kwa upande wa huduma ndogo ya fedha serikali imeweka mkazo na mazingira wezeshi kwa kupitia sheria ,sera,ptogram na mipango mbalimbali na kuyoa fursa kwa taasisi ya elimu kufanya tafiti na kushiriki moja kwa moja katika kuiwezesha jamii kuwa na maarifa na ujuzi wa masuala ya fedha kwa makundi mbalimbali ikiwemo makundi ya wanafunzi,makundi maalum ya wanawake,vijana na wenye uhitaji maalum ,watoto,wajasiriamali wadogo nawa kati na jamii kwa ujumla.
0 Comments