Header Ads Widget

VIONGOZI WA JUMUIYA YA MARIDHIANO WAISHUKURU HOSPTALI YA BENJAMINI MKAPA

 


 

Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma


VIONGOZI wa Jumuiya ya Maridhiano mkoa wa Dodoma wamepaza sauti zao kwa kuishukuru serikali na Taasisi ya Benjamini Mkapa kwa kuendelea kutoa huduma mbalimbali kwa jamii.


Akiongea kwa niaba ya viongozi wazake Askofu Evance Chande, ambaye ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Karmeli Assemblies of God na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano Mkoa wa Dodoma amesema lengo la mkutano huo ni kuishukuru Hospitali ya Benjamini Mkapa.


Askofu Evance alitumia rejea katika Biblia kutoka kitabu cha Luke 17:12-19 kuishukuru serikali ya awamu ya sita na Hospitali akisema yeye alihudumiwa vizuri, kwa kupewa maneno yenye faraja kutoka kwa watumishi.


“Nilipaswa niende India, kama serikali isingewekeza hapa huenda nisingekuwepo leo maana ugonjwa ulikuja ghafla, ingekuwa vigumu kukusanya fedha na kuwahi matibabu hayo nje ya nchi” Askofu  Chande.


Kwa upande wake Katibu wa BAKWATA Mkoa wa Dodoma Shekhe Hussein Ramadhani Kuzungu, ametoa ushuhuda wa namna alivyopokea matibabu baada ya kupata ajali, akisifia kauli nzuri na kutoa wito kwa wanadodoma kujivunia uwekezaji wa Serikali katika Hospitali ya Benjamin Mkapa.


“Tunaona kwenye mtandao, tunashuhudia tukifika, wewe ni Mkurugenzi unayejitambua, hukai ofisini na unao watumishi wenye kauli nzuri wanatujenga kiimani” Sheikhe, Kuzungu.


Naye Dkt, Alice Kaijage, Mwakilishi wa Wafanyakazi Bungeni ambaye alifurahishwa na taarifa Chanya kutoka kwa viongozi wa dini kwenda kwa wafanyakazi. 


“Ninawashukuru kwa jinsi mnavyoishi viapo vyenu, BMH mmenifariji sana, mmmemvisha Ua Mheshimiwa Rais, mmeithaminisha serikali na Chama cha Mapinduzi” Amesema  Dkt. Kaijage. 


Amesema Benjamin Mkapa ni Hospitali inayotoa huduma za Uchunguzi na Matibabu ya kibingwa na Ubingwa bobezi hasa zile zilizokuwa adimu nchini.


Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kati Benjamin Mkapa (BMH)Dk Alphonce Chandika  amewaomba viongozi wa dini kuendelea kuwaombea wagonjwa na watoa huduma za Afya nchini akisema kwa sababu madaktari wanaweza kutibu lakini mwenye uwezo wa kuponya ni Mungu pekee.

 

Dkt. Chandika ameyasema hayo leo alipotembelewa na ujumbe wa Jumuiya ya Maridhiano ya Mkoa wa Dodoma uliyofika Hospitalini hapo kutoa pongezi maalumu za kutambua mchango wa Hospitali hiyo katika utoaji wa huduma wenye kujali utu na kumfariji mgonjwa.


“Moyo wangu umejaa furaha sana kuwasikia mkitambua mchango wetu na wa serikali kufanya uwekezaji katika sekta ya Afya, ninaomba muendelee kutuombea wafanyakazi wa sekta ya Afya na wagonjwa kwani sisi tunachofanya ni kutibu tu, Mungu ndiye anaponya” Amesema Dkt. Chandika.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI