Header Ads Widget

PROF. MKENDA AISHUKURU NBC KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI ELIMU NA UJUZI KWA VIJANA

 



Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma


WAZIRA wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda ameishukuru  Benki ya NBC kwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika jitihada za kutoa Elimu na ujuzi kwa vijana hapa nchini katika kukabiliana na tatizo la ajira hasa kwa vijana wanapofika umri wa kujitegemea. 


Hayo ameyasema jijini Dodoma Kwenye  hafla ya utiaji saini Mkataba wa Makubaliano na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa ajili ya ufadhili wa wanafunzi 1,000 wa Vyuo vya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) ikiwa ni Mkakati wa Benki ya NBC  kukuza ujuzi kwa vijana ili waweze kujiari wenyewe.


Waziri Mkenda amesema NBC kuja na mpango huo unakwenda kusaidia mkakati wa Serikali katika kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.


" Ufadhili huo unakwenda kutimiza azma ya Serikali ya kutoa Elimu na Mafunzo yatakayo wawezesha vijana wa kitanzania kupata ujuzi wa kujiajiri ama kuajiriwa," Amesema Waziri Mkenda


Na kuongeza" Niwahakikishie Benki ya NBC kuwa Wizara hiyo itatengeneza mfumo wa uwazi wa matumizi ya fedha hizo ili ziweze kutoa matokeo yaliyokusudiwa katika kuwajengea ujuzi vijana ili waweze kujitegemea badala ya kusubiri kuajiliwa pekee," amesema


Aidha ameeleza kuwa kupitia mpango huo wataainisha maeneo yenye uhitaji zaidi au yenye fulsa nyingi za vijana kujiajiri wenyewe na maeneo hayo yatapewa kipaumbele zaidi katika mpango huo.


Ameongeza kuwa “Makampuni yanayoanzishwa hasa katika Mkoa wa Pwani niwatake tu VETA kwa kushirikiana na Katibu Mkuu kukaa na uongozi wa Mkoa wa  Pwani na kuwakutanisha makampuni yanayoanzisha viwanda ili kubaini maeneo ya ujuzi yanayohitajika Zaidi ili tuzalishe wataalamu wengi” amesema.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) CPA Anthony Kasore ameishukuru Wizara kwa kuwezesha kupatikana ufadhili huo kutoka Benki ya NBC ambao utawezesha Vyuo hivyo kutoa Mafunzo ya Ujuzi kwa vijana wengi.


CPA Kasore amesema kuwa VETA imepokea Mradi huu pamoja na maelekezo ya kuhahakisha zinatumika kwa uwazi na kwa kutoa mafunzo yenye uhitaji na kuleta matokeo chanya kwa haraka.


 ''Mradi huo utaleta tija na kuahidi kuwazi katika upatikanaji wa vijana wanaotakiwa ili mradi huo uweze kuleta tija iliyokusudiwa na maagizo yote yatatekelezwa kama inavyotakiwa.''amesema CPA Kasore


Awali  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Theobald Sabi amesema Benki hiyo itatoa kiasi cha shilingi Milioni 100 kwa ajili ya kufadhili vijana 1000 watakaokwenda kusomea kozi katika Vyuo Mbalimbali vya VETA hapa nchini.


“Mpango huu unaitwa NBC Wajibika Scholarship tunatambua tatizo la ajira kwa Vijana na ni kilio cha Dunia nzima kupitia ufadhili huu tutatoa ufadhili kwa vijana 1000 na huu ni mwanzo tu idadi itakuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka tunaamini hawa wakiweza kujiajiri tutakuwa tumepunguza kwa kiasi flani” amesema Sabi.


Ametaja baadhi za kozi zitakazofadhiliwa kuwa ni Ushonaji, Uselemara, Ufundi wa Magari, Ufundi Ujenzi, Upambaji na kozi nyingine tutakazobaini zina fulsa nyingi kwa vijana kujiari na kuendesha maisha yao.


Ameongeza kuwa “ Mbali na ufadhili huu Benki itawaingiza vijana hao 100 katika mpango maalumu wa Elimu ya Fedha ujulikanao kama NBC Busness Club na tutaweza kuwafungulia akaunti Maalumu zijulikanazo kama NBC Kuwa Nasi Akaunt zisizokuwa na makato yoyote ili wajiwekee akiba” amesema.


Amesema ufadhili huo utaratibiwa na Wizara ya Elimu na kutekelezwa na Vyuo vya Ufundi Stadi VETA na NBC itaendelea na dhamira yake ya kuwa mdau muhimu wa elimu na uwezeshaji wa vijana.


Amesema kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita NBC imewekeza kiasi cha shilingi milioni 350 katika kutoa ufadhili wa vijana 70 wa ngazi za elimu ya juu, na imekuwa ikishiriki katika ujenzi na ukarabati wa miondombinu ya shule mbalimbali hapa nchini.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI